Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuchezwa wikiendi ya mwisho wa mwezi Machi mwaka huu, huku timu nane zikichuana kusaka nafasi ya kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Machi 26, 2016 utachezwa mchezo mmoja ambapo Wachimba dhahabu wa Geita Gold watakua wenyeji wa wachimba Almasi wa mkoa wa Shinyanga timu ya Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kirumba.
Alhamisi ya Machi 31, 2016, Young Africans watawakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku timu ya Azam FC wakiwa wenyeji wa maafande wa jeshi la magereza Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mchezo wa mwisho wa robo fainali utachezwa Aprili 6, 2016 kwa Simba SC kucheza dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Aprili 7, 2016 itachezeshwa droo ya hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) mojamoja (live) katika Luninga.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu, ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) 2017.
0 maoni:
Chapisha Maoni