Mechi ambayo imeisha kwa magoli 2-2 na kuipa nafasi nzuri Leicester City kama wakishinda mechi ya leo dhidi ya Watford imefanyika kwenye uwanja wa White Hart Lane. Wakati mechi inaendelea ndani nje kulikua na fujo kati ya mashabiki na polisi ambapo chanzo kamili cha fujo hizo hakijajulikana ni nini.
Fujo hizo zilipelekea hadi mashabiki wengine kupasuka na kuanza kutoka damu hata kabla hawajaingia ndani ya uwanja.Kutokana na fujo hizo polisi walitumia hadi farasi kuleta utulivu eneo la tukio ili mambo yaende kama yalivyopangwa. Mwisho wa siku mechi imeisha, mashabiki wameumizwa lakini ndio uhalisia kwenye viwanja vingi vya michezo lazima watatoke watu wanaotaka kuvunja amani.
0 maoni:
Chapisha Maoni