Itachukua miezi sita kudhibiti Ebola
Mkuu wa shirika la madaktari wasio na mipaka la Medicins Sans
Frontieres, amesema kuwa itachukua miezi sita kuweza kudhibiti janga la Ebola
katika mataifa ya Afrika Magharibi.
Akizungumza mjini Geneva,mkuu huyo, Joanne Lui alisema kuwa uongozi mzuri
unahitajika kutoka kwa shirika la afya duniani na kwamba kukabiliana na Ebola
hasa ilikozuka mwanzo nchini liberia, ni muhimu zaidi katika kumaliza ugonjwa
huo.Hasa amesisitiza kwamba wataalamu zaidi wenye uzoefu wa kupambana na ugonjwa hupo wanahitajika katika maeneo yaliyoathirika.
Bi Lui aliongeza matabibu 80 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, huku watu wengine 170 wakiambakizwa na kwamba nyingi ya vituo vya afya vimefurika wagonjwa wa Ebola.
''Ikiwa hatutapambana na ugonjwa huo nchini Liberia,basi itakuwa vigumu kuudhibiti katika kanda nzima ya Afrika Magharbi,'' alisema Bi Lui.
Mifumo ya afya katika neo la Afrika Magharibi inakabiliwa na hali ngumu wakati huu wa mlipuko wa Ebola.
Ebola huambukizana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, kupitia maji maji ya mwili au damu.
Dalili kama za mafua zinaweza kusababisha mtu kuvuja damu kutoka kwenye sehemu zake za mwili kama vile masikioni, mapuani, machoni na ndani ya mwili na kusababisha viungo vya mwili kutofanya kazi.
0 maoni:
Chapisha Maoni