Wachimba migodi wakumbuka Marikana
Maelfu ya wachimba migodi wa Afrika Kusini
wamekusanyika katika mgodi wa dhahabu nyeupe wa Marikana nje ya
Johannesburg kukumbuka mwaka wa pili tangu wenzao 34 kuuliwa na polisi.
Viongozi kadha wa upinzani piya walikuwamo katika mkusanyiko huo.Uchunguzi unaofanywa na wanasheria kuhusu mauaji hayo bado unaendelea.
Jumatatu, naibu rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, alitokeza mbele ya tume hiyo.
Bwana Ramaphosa alikuwamo kwenye bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Lonmin wakati wa mauaji hayo.
0 maoni:
Chapisha Maoni