KOCHA MPYA, GUNDU PALE PALE MAN UNITED, YAFUMULIWA 2-1 NA SWANSEA OLD TRAFFORD UFUNGUZI LIGI KUU ENGLAND
KOCHA mpya matatizo yale yale Manchester United- hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mashetani hao Wekundu kuanza vibaya Ligi Kuu ya England kwa kuchapwa mabao 2-0 na Swansea City Uwanja wa Old Trafford.Mabao yaliyomfanya kocha Mholanzi, Louis Van Gaal aanze vibaya Ligi Kuu yamefungwa na Ki dakika ya 28 na Sigurdsson dakika ya 72, wakati Nahodha Wayne Rooney aliifungia United dakika ya 53.
Kikosi cha Man Utd kilikuwa; De Gea; Jones, Smalling, Blackett, Lingard/Januzaj dk24, Fletcher, Herrera/Fellaini dk67, Young, Mata, Hernandez/Nani dk46 na Rooney.
Swansea; Fabianski; Rangel, Amat, Williams, Taylor/Tiendalli, Ki, Shelvey, Routledge, Sigurdsson, Dyer/Montero dk67 na Bony/Gomis dk77.
Matatizo pale pale; Kocha Van Gaal kulia na Msaidizi wake, Ryan Giggs kushoto wakiwa hawaamini macho yao
0 maoni:
Chapisha Maoni