Jumapili, 8 Februari 2015

Uchunguzi wa suala la kuundwa mahakama ya jinai za kivita CAR

Wawakilishi wa Baraza la Taifa la Mpito (Bunge) katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) wameitisha kikao cha dharura kitakachojadili rasimu ya katiba mpya kwa muda wa siku 15. Miongoni mwa maudhui muhimu za rasimu hiyo ni suala la kuundwa mahakama maalumu ya jinai za kivita zilizofanyika nchini humo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Kwa uchache watu 5000 waliuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuwa wakimbizi katika mgogoro wa kisiasa na mauaji ya kikaumu ya miaka miwili ya hivi karibuni katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Takwimu zinaonesha kuwa, Waislamu ndiyo wahanga wakubwa zaidi wa mapigano yanayojiri kati ya wanamgambo wenye misimamo mikali wa Kikristo wa Anti-Balaka na wale wa Seleka. Mashambulizi ya wanamgambo wa Anti-Balaka katika maeneo ya Waislamu yalilazimisha idadi kubwa ya Waislamu hao kukimbilia katika nchi jirani kwa kuhofia maisha yao. Ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa yenye kurasa 127 iliyotolewa mwezi jana, ilizituhumu pande mbili kuwa zilihusika na mauaji ya raia wasio na hatia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ripoti hiyo pia imelituhumu jeshi la serikali na wanamgambo wa Muungano wa Seleka na wale wa Anti-Balaka, kuwa walifanya mauaji, kuwatumikisha watoto katika mapigano ya silaha, ubakaji na uporaji wa mali za wananchi.
Mauaji ya maelfu ya watu katika mapigano ya ndani nchini humo, yalifanyika baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013 na hadi sasa hakujatolewa takwimi kamili kuhusu idadi ya watu waliouawa katika machafujo hayo. Wanamgambo wa Anti-Balaka wanamtuhumu Michel Djotodia, aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya François Bozizé, kuwa ndiye mhusika wa jinai za kivita na ukikwaji wa haki za binadamu uliofanyika katika nchi hiyo iliyoko katikati mwa Afrika. Djotodia aliyekuwa kuwa Rais wa serikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, alilazimika kujiuzulu nafasi hiyo baada ya mauaji ya umati yaliyofanywa dhidi ya Waislamu. Jinai za mauaji ya Waislamu zilizoambatana na kuwalazimisha makumi ya maelfu ya wengine kuwa wakimbizi, zilifanyika katika hali ambayo kulikuwepo vikosi vya kusimamia amani vya Umoja wa Mataifa na askari wengine 2000 wa Ufaransa nchini humo. Mwezi Aprili mwaka jana Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio la kutumwa askari wa nchi mbalimbali chini ya mwamvuli wa kikosi cha MINUSCA nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Majukumu ya kikosi hicho ni kulinda usalama wa raia, kusaidia serikali ya mpito, kuwasilisha misaada kwa wakimbizi, kuyapokonya silaha makundi yanayopigana na kuimarisha jeshi la serikali. Askari hao wa kimataifa ambao hadi mwanzoni mwa mwaka huu idadi yao ilifikia elfu 12, waliungana na wenzao 6200 wa Kiafrika.
Kinyume na madai ya Ufaransa, karibu askari 2000 wa nchi hiyo ambao wamekuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwezi Januari mwaka 2013, hawajasaidia lolote katika kurejesha usalama na amani katika nchi hiyo. Badala yake askari hao wa Ufaransa wamechochea zaidi machafuko kwa kuwapendelea wapiganaji wa Kikristo wa Anti-Balaka dhidi ya Waislamu.
Ni kwa kuzingatia ukweli huo, ndiyo maana suala la kuundwa mahakama maalumu ya kuchunguza jinai zilizofanywa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita nchini humo likawa na umuhimu mkubwa zaidi.
Zaidi katika kategoria hii: 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Uchunguzi wa suala la kuundwa mahakama ya jinai za kivita CAR Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top