Jumapili, 8 Februari 2015

YANGA YALIPA KISASI KWA MTIBWA, YAJIKITA KILELENI

Timu ya Yanga ya DSM imefanikiwa kulipa kisasi cha mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa mzunguko wa Pili wa Ligi Kuu Tanzania bara uliopigwa leo katika dimba la Taifa.
Katika mchezo wa mzunguko wa Kwanza uliopigwa mwaka jana, Yanga iliyokuwa chini ya Marcio Maximo ilifungwa na Mtibwa mabao 2-0 katika dimba la Jamhuri Morogoro, kwahiyo ushindi wa leo ni kisasi kwa Mtibwa iliyo chini ya nahodha wa zamani wa Taifa Stars Meck Mexime.
Mrisho Khalfan Ngassa ndiye aliyewainua mashabiki wa Yanga dakika ya 55 ikiwa ni dakika moja baada ya kuingia akichukua nafasi ya mliberia Sherman ambaye katika mchezo wa leo alionesha kiwango cha chini tofauti na matarajio ya wengi.
Ngassa ambaye ndiye aliyeipa Yanga uhai kimchezo baada ya kuingia, alifunga bao la Pili katika dakika ya 62 na kuihakikishia Yanga point 3 muhimu na kufanya ifikishe point 25 kileleni mwa msimamo wa ligi ikifuatiwa na Azam yenye point 22 na Mtibwa imeendelea kubaki nafasi ya 6 na point zake 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: YANGA YALIPA KISASI KWA MTIBWA, YAJIKITA KILELENI Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top