Jumapili, 2 Novemba 2014

TUWE AMA TUSIWE NA RANGI YA NGOZI SOTE NI NDUGU (sote ni ndugu mmoja)! KILIO KILA SIKU HATUHEMI!

Ulemavu wa ngozi ni tatizo linalorithiwa kutokana na ukosefu wa pigment katika nywele, ngozi na macho.



Ni tatizo linalowapata watu bila kujali kabila wala jinsia. Huko Marekani na Ulaya inakadiriwa kwamba mtu mmoja kati ya 20,000 huwa na dalili za ulemavu wa ngozi, wakati hapa kwetu Tanzania takwimu zinaonyesha kuwa mmoja kati ya watu 4,000 ana dalili za ulemavu huo
 Kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) Tanzania ina walemavu wa ngozi takriban 170,000.



Tangu mwaka 2007, Tanzania imekuwa ikishuhudia mauaji ya kikatili ya albino ambayo yanahusishwa na ukataji wa viungo mbalimbali vya miili yao ambapo watu  74 wameumizwa vibaya na kati yao 62 waliuawa na 12 wakabaki na madonda mabaya wengine wameachwa wakiwa hawana baadhi ya viungo vyao vya mwili baada ya kukatwa na kunyofolewa kikatili.
 Kati ya sababu zinazotajwa kupelekea unyama huu ni imani za kishirikina kuwa baadhi ya viungo vya mwili wa albino vina uwezo wa kuleta utajiri.



Serikali ya Tanzania imefanya jitihada nyingi kukabiliana na tatizo hili ikiwa ni pamoja na kusitisha shughuli za waganga wa jadi ambao inasemekana ndio wanaochochea ukatili huu.

Pia serikali imeagiza kamati za ulinzi za mikoa kuwalinda albino na imeendesha upigaji wa kura za maoni kwa siri nchi nzima ili kuwabaini wahusika.




Zaidi ya hayo, vyama vya kiraia, vyombo vya habari na hata taasisi za nje pia zimechangia sana katika kampeni hii ya kutokomeza mauaji haya ya kinyama.




Tarehe 4 May ni siku ya Albino duniani. Siku ya albino duniani ni siku tunayotumia kuendeleza kuhamasisha juu ya kuelewa zaidi kuwepo kwa wenzetu wasio na rangi ya ngozi na jinsi ya kushirikiana nao kuyatatua matatizo yanayoambatana na hali hii
 Katika kuonyesha masikitiko yao juu ya hali inayowakabili albino, wanaharakati wakiongozwa na Chama cha Albino nchini (TAS) waliandamana jijini Dar es salaam Oktoba 19 wakilaani mauaji hayo.
Maandamano yaliyopokelewa na Rais Jakaya Kikwete yalimpa fursa ya kukemea mauaji hayo na kuahidi serikali kukabiliana na wauji kwanguvu zake zote.
Katika hotuba yake rais alisema kuna jitihada za kukabiliana na mtandao unaojihusisha na mauaji na kuwataka wananchi kusaidiana na polisi katika vitahivyo. Mauaji hayo ya kutisha yanajitokeza wakati kuna hekaheka za wanaharakati kutaka hukumu ya kifo ikomeshwe nchini
Kwa sasa, sheria inaruhusu mtu yoyote anayefanya kosa la kumuua mwingine, kama inavyotokea kwa mauaji ya albino, na yeye pia kuuawa kwa kunyongwa.




Kulingana na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, bado Tanzania inaendeleza hukumu ya kifo katika makosa yanayohusiana na uhaini na mauaji.

Rwanda, moja ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikomesha adhabu ya kifo Julai 25, 2007.

Suala la hukumu ya kifo lilizua mjadala mkali lilipoibuliwa katika vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Januari mwaka huu, huku kukiwepo na hoja za kuunga mkono kukomeshwa na nyingine zikitaka kuendelezwa kwa hukumu hiyo.
 Wale waliotaka kutungwa kwa sheria inayounga mkono kukomeshwa kwa hukumu ya kifo walitoa sababu za ugumu na uzito wa kutekeleza adhabu hiyo hususani kwa mamlaka ya mwisho ya kusaini hati ya kumnyonga mwenye hatia. Pia walikuwa na msimamo kuwa tendo la kuua ni la kikatili na mara nyingi kuna ucheleweshwaji wa adhabu yenyewe.



Walisema mamlaka ya kutoa uhai wa mtu ni ya Mungu hivyo kuwepo na haja ya kutunga sheria ya kufuta hukumu hiyo. Hata hivyo, upande wa serikali uliendelea kushikilia msimamo wake wa kuendeleza hukumu hiyo huku naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, akipinga dhana kuwa adhabu hiyo
Mwajuma Ismail yeye ni mlemavu wa ngozi, anasema, anapata mashaka juu ya maisha yake kwani anaamini muda na wakati wowote binadamu asivyo na roho ya huruma anaeza kukatisha maisha yake
Alizungumza kwa uchungu huku akisema ana mtoto mwenye umri wa miaka 8 ila amemkatisha masomo kuhofia atafanyiwa vitendo vya kikatili kutokana na umbali wa makazi ya nyumba yake na anakosoma mwamae huyo
Baltazary Kweka ni mwenyekiti katika kijiji cha mulama kinachopatikana kata ya narumu mkoani Kilimanjaro ambapo kijiji hicho kina zaid ya malemavu 40,eye  alisema kuwa wamefanya kila jitihada  kuhimiza wazazi wa watoto wenye ulemavu wa ngozi kuwapeleka shule ila wameangukia pua kutokana n ahofu kutanda kila kukikucha dhidi ya watoto hao
 Jamii nayo haifurahii vitendo vya kikatili vinavyofanywa na baadhi ya watu japo wanaofanya wanatoka humo humo ndani ya jamii
Veronica  Chami ni mmoja wa mwanafunzi anayesoma katika shule zilizo ndani ya kijiji cha narumu watokapo akina Mwajuma Ismail na mwanae yeye anasema anapata uchungu anapoona wenzake wenye ulemavu wa ngozi wanaishi kwa mashakahuku baadhi yao wakikatishwa masomo
‘Wauaji wapo huku huku ndani ya jamiii sema ndo hivyo hatuwajui,siku zote kikulacho ki nguoni mwako” alisema veronica kwa uchungu mkubwa


Tuwaite albino?
Wanadamu wasio na rangi ya asili (melanin) tunawaita albino ambalo ni jina la Kiyunani linalomaanisha rangi
Jina hili halielezi ya kutosha hali hii kwani kusema tu albino yaani rangi haitoi maana yeyote. Hata hivyo kwa sababu tumeishawahi kulisikia mara nyingi na tumewaona albino, mtu akilisema tunajua anachosema. .
Watu hawa wenye ulemavu wangozi mara nyingi wamekuwa waiitwa majina mbalimbali kama vile zeruzeru huku baadhi yao wakikasirika kutokana na majina wanayoitwa.


Jina lingine tunalosikia ni ‘ulemavu wa rangi ya ngozi.’ Hapa kuna tatizo la kuwa jina hili linasisitiza sana kuwa hali hii ni ya ulemavu kiasi cha kuwafanya wahusika wajisikie ‘sisi ni walemavu.’
 Hakuna sababu ya kusisitiza kuwa huu ni ulemavu kwani kwa mfano katika hali nyingine za kurithi hatukutaja kuwa zinaitwa ulemavu.
Lakini kwa ndugu zetu wasio na rangi ya ngozi ni kwamba hiyo rangi haipo kabisa.Sasa unawezaje kusema kitu ni kilemavu wakati hakipo.

Ingekuwa wewe ndio mlemavu wa ngozi ukafanyiwa vitendo vya kikatili ungejisikiaje? Wasomaji, wataalamu na Wasio na Rangi ya Ngozi, Macho na Nywele nipeni   maswali na maoni yenu 
0757547000

Mauaji dhidi ya walemavu wa ngozi (albino) yazidi Tanzania




Nchini Tanzania, kesi za ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi, yaani albino, zimefikia 151, na kusababisha vifo vya watu 74, wengine wakilemazwa.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa na Alicia Londono, mtalaam wa ulemavu huo katika ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa aliyehitimisha ziara yake nchini Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Geneva, ameeleza wasiwasi wa ofisi hiyo juu ya kuzidi kwa mashambulio dhidi ya Albino kwa misingi ya ushirikina na pia biashara ya viongo vya mwili.
(Sauti Alicia)
“Matukio mengi ya kushambuliwa kwa albino yanafanyika vijijini ambako imani zimejikita sana miongoni mwa jamii ikiwemo mamlaka za kusimamia sheria. Waathirika wanapata mkwamo kufikisha kesi zao mbele ya sheria kwa sababu wanajihisi kutengwa na jamii.Na kwenye matukio mengi, familia au jamii wanahusika na hivyo ni vigumu kupata mashahidi na hawapati usaidizi wowote kama vile kuelimishwa kuhusu haki za kisheria au msaada wa kisheria.”
Amesema, walemavu hao pamoja na kuathirika kiafya, huwa hatarini kufariki dunia mapema kwa sababu hawajui jinsi ya kujikinga na saratani ya ngozi, wanakabiliana na unyanyapaa na ukatili. Wengi wao wanatelekezwa na wazazi wao.
Aidha, amesema ripoti ya ofisi ya haki za binadamu inaonyesha kuwa jibu la polisi la Tanzania haitoshi licha ya serikali kuunda jopo maalum la kufuatilia kesi hizo.
Hatimaye, amesema vituo vya kulinda watoto walioshambuliwa ama waliotelekezwa na wazazi wao vinahitaji misaada ili kuimarisha huduma zao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: TUWE AMA TUSIWE NA RANGI YA NGOZI SOTE NI NDUGU (sote ni ndugu mmoja)! KILIO KILA SIKU HATUHEMI! Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top