ANGALIA PICHA ASKARI AMKATA VIDOLE VINNE MFANYAKAZI WAKE
JESHI la
Polisi mkoani Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma wa Kituo cha
Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la kumjeruhi mtumishi wake wa
ndani kwa mkumkata vidole vyake vinne vya mkono wa kulia kwa panga,
akimtuhumu kumwibia Deki ya Video nyumbani kwake.
Tukio
hilo la kujeruhiwa kijana Steven Magessa (18), lilitokea Oktoba 20 mwaka
huu katika kijiji cha Magange Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara
nyumbani kwao kijana huyo aliyekuwa amekimbilia huko baada ya kudaiwa
kumwibia mwajili wake nyumbani eneo la Igogo.
AKIONYESHA NAMNA ALIVYOJERUHIWA NA MAMA HUYO
Akizungumza na waandishi wa habari kijana huyo alieleza kuwa kufanya kazi kwa askari huyo kulikuja mara baada ya askari huyo kumfuata kijijini na kumuomba ridhaa ya wazazi wa kijana huyo kuambatana naye jijini Mwanza ili kumsaidia kazi za nyumbani ambapo walikubaliana malipo ya kiasi cha Sh 50,000/= kila mwezi jambo ambalo askari huyo alilikiuka na kushindwa kulitekeleza kwa muda wa miezi sita bila kumlipa mshahara
0 maoni:
Chapisha Maoni