YANGA YAICHAPA MGAMBO 2-0
Young
Africans imebuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya JKT Mgambo ya
jijini Tanga mchezo uliofanyika jioni ya leo dimba la Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam, huku Saimon Msuva akibuka shujaa kwa kukwamisha
wavuni mabao yote mawili.Young
Africans iliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka mabao ya mapema,
lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake Jaja, Coutinho na Ngasa
kulipelekea kukosa mabao ya wazi dakika 45 za kipindi cha kwanza na
kufanya timu kwenda mapumziko zikiwa 0-0.Kipindi
cha pili Young African illifanya mabadiliko kwa kuwatoa Haruna
Niyonzima na Geilson Santos "Jaja" na nafasi kuchukuliwa na Saimob Msuva
na Jerson Tegete ambao waliongeza kasi ya mchezo na mashambulizi
langoni mwa Mgambo JKT.
Dakika
ya 74 ya mchezo, Saimo Msuva aliipatia Young Africans bao la kwanza
baada ya kuitendea vyema pasi ndefu ya kiungo Mbuyu Twite aliyompenyezea
na kumkuta mfungaji ambaye aliudokoa mpira huo na kujaa wavuni na
kumuacha mlinda mlango wa Mgambo JKT Said Lubawa akigaa bila ya jujua
cha kufana.
Baada
ya bao Mgambo JKT walicharuka na kufanya mashambulizi kadhaa langoni
kwa Young Africans kwa lengo la kusaka bao la kusawazisha, lakini
mashambulizi yao yalikuta yakiokolewa na na walinzi wa Young Africans
pamoja na mlianda mlango Deo Munish "Dida"
Huku
baadhi ya washabiki wakianza kutoka nje wakijua mchezo umemalizika kwa
ushindi wa bao 1, Saimon Msuva tena aliipatia timu yake ya Young
Africans bao la pili baada ya pasi aliyotanguliziwa na kiungo Hassan
Dilunga kuitumia vyema na kuachikia shuti lililojaa wavuni moja kwa
moja.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizka, Young Africans 2 - 0 Mgambo JKT.
Kwa
ushindi wa leo Young Africans inakamata nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC
iliyoko nafasi ya pili huku wakiwa sawa kwa kwa point na mabao ya
kufunga na kufungwa, Mtibwa Sugar wakiendelea kushika nafasi ya kwanza.
Young Africans:
1. Deo Munish "Dida", 2. Juma Abdul. 3.Oscar Joshua/Hamis Kizza,
4.Rajab Zahir, 5.Kelvin Yondani, 6.Mbuyu Twite, 7.Hassan Dilunga,
8.Haruna Niyonzima/Saimon Msuva, 9.Geilson Santos "Jaja". 10.Mrisho
Ngasa, 11.Andrey Coutinho
0 maoni:
Chapisha Maoni