Mataifa ya Magharibi waishtumu Urusi
Mataifa ya Magharibi yameshtumu kwa hasira kuingia kwa msafara
wa malori ya misaada kutoka Urusi katika eneo linalodhibitiwa na waasi
mashariki mwa Ukraine.
Marekani na Ujerumani zimetaja kitendo hicho kama hatari na kwamba kuna hofu
huenda Urusi ikatumia hatua hiyo kama sababu ya kuivamia Ukraine.Awali NATO ilikuwa imesema kuwa Urusi inasafirisha silaha kali kuingia nchini Ukraine na kwamba imekuwa ikitumia mizinga yake ndani ya ardhi ya Ukraine dhidi ya vikosi vya Ukraine.
Hatahivyo Urusi inasema kuwa msafara huo umebeba maje-nereta, chakula na maji,lakini waandishi walioona malori hayo wanasema kuwa yamebeba mizigo nusu na kwamba Ukraine inasema kuwa msafara huo unatumiwa kuwasaidia waasi wanaounga mkono Urusi katika eneo la mashariki.
0 maoni:
Chapisha Maoni