KIPA KIBOKO YA AZAM KAGAME AENDELEZA MAAJABU YA PENALTI KIGALI, MERREIKH YAITUPA NJE KCC YA BRIAN UMONY
KIPA kinda wa miaka 19 wa Uganda, Magoola Omar Salim aliyewatoa Azam FC katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame juzi- leo amekuwa tena shujaa wa timu yake, El Merreikh Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda.Mlinda mlando huyo wa U20 ya Uganda ‘Thw Kobs’, ameiwezesha Merreikh kwenda Fainali ya Kagame kwa ushindi wa penalti 3-0, kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 120.
Magoola aliokoa penalti za Brian Umony na Brian Majwega wakati ya Tom Masiko iliota mbawa-na Alan Wanga alipoteza penalti upande wa Merreikh.
Magoola alikwenda kupiga penalti ya mwisho ya Merreikh na kufunga baada ya wenzake Ballah Gabril na Faisal Hussein kufunga pia.
Dakika 90 zilimalizika tayari timu hizo zikiwa zimekwishafungana mabao 2-2, ya KCC yakifungwa na Tom Masiko dakika ya 32 na Brian Umony dakika ya 82, wakati Merreikh yalifungwa na Mohammed Traore dakika ya 32 na Ragi Abdallah dakika ya 69.
Hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao katika dakika 30 za nyongeza na mchezo ukaenda kumalizikia kwenye mikwaju ya penalti.
Kipa huyo, juzi alidaka penalti ya Lionel Saint- Preux wa Azam FC katika mchezo wa Robo Fainali, El Merreikh ikishinda kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
Sasa Merreikh wanasubiri mshindi kati ya timu za hapa, Polisi na APR kwa aili ya Fainali Jumapili Uwanja wa Amahoro.
0 maoni:
Chapisha Maoni