Jumanne, 24 Desemba 2013



Taarifa zaidi kuhusu ndege ya British airways iliyogonga jengo huko South Africa

Moja kati ya ndege za Shirika la ndege la British Airways Boing 747 inayokadiriwa kuwa na abiria 189 imepata ajali wakati inajiandaa kupaa baada ya moja ya bawa lake kugonga jengo lililokaribu na uwanja wa ndege wa OR Tambo Johannesburg South Africa.

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea London Uingeleza na baada ya kupata ajali hiyo abiria wote walishushwa salama na kupelekwa hotelini,mpaka sasa inasemekana ndege hii imeingia dosari japo bado haijathibitishwa vizuri.

Mwanahabari Harriet Tolputt ali-tweet tuhuma kuhusu ajali hiyo baada ya abiria wa daraja la kwanza kuanza kushushwa kwanza na kisha abria wa madaraja mengine kusubiri kitu ambacho hakikua kizuri hasa kwa wakati wa dharura kama ile.

Harriet Tolputt aliandika ‘Abiria yeyote ambaye yupo karibu na mlango wa dharura anaweza kutoka bila kujali daraja lake kwa sababu ni muda wa hatari ndege ikiwa imegonga sehemu kama ile’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top