Jumanne, 24 Desemba 2013

            Messi amshambulia Rais wake

STAA wa Barcelona, Lionel Messi, amemshambulia Makamu Rais wa Barcelona, Javier Faus, kufuatia kauli yake kwamba staa huyo wa Argentina hatapatiwa mkataba mnono kwa haraka kama inavyosemwa.

Kumekuwapo na ripoti nyingi kuwa staa huyo anataka kulipwa mshahara mnono zaidi klabuni hapo na hivyo kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi La Liga baada ya Cristiano Ronaldo kumpiku katika miezi ya karibuni.

Hata hivyo, Messi amemshambulia Faus huku akisisitiza kwamba hajawahi kuulizia mkataba mpya wa pesa nyingi na kudai kuwa Faus hana uelewa mkubwa na masuala ya soka.

Faus ni mtu ambaye hajui lolote kuhusu soka. Anajaribu kuiendesha Barcelona kama biashara, lakini hii ni klabu ya soka. Barcelona ni klabu bora duniani na lazima iwe na wakurugenzi bora duniani. Sijawahi kuulizia mkataba mpya na wala wawakilishi wangu hawajawahi kufanya hivyo,” alisema Messi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top