Chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD kimemtuhumu Rais Paul Kagame wa Rwanda kuwa anataka "kusafirisha" mauaji ya kimbari, huku uhusiano kati ya nchi mbili hizo jirani ukizidi kuharibika.
Kiongozi wa chama tawala cha Burundi Pascal Nyabenda ambaye pia ni Spika wa Bunge la nchi hiyo amesema: "maabara ya mauaji ya kimbari iko Rwanda kwa sababu baada ya Rais Kagame kuyafanyia majaribio huko, anataka kuyasafirisha kuyaleta Burundi ili awe na nafasi ya kuwa beberu mdogo".
Uhusiano baina ya mataifa hayo ya eneo la Maziwa Makuu umeshuka hadi kiwango cha chini huku Burundi na Umoja wa Mataifa zikiilaumu Rwanda kuwa inawaunga mkono waasi wa Burundi.
Kiongozi huyo wa chama tawala cha Burundi amelikosoa pia Kanisa Katoliki ambalo hivi karibuni lilitoa wito wa kufanyika mazungumzo baina ya Kigali na Bujumbura ili kupunguza moto wa mgogoro unaozidi kutokota.
Burundi imekumbwa na mgogoro wa kisiasa tangu Aprili mwaka jana wakati Rais Pierre Nkurunziza alipoamua kugombea tena urais kwa muhula wa tatu, na kushinda katika uchaguzi huo uliofanyika mwezi Julai.
Watu wapatao 400 wameuawa hadi sasa na wengine wapatao laki mbili na nusu wameihama nchi na kuwa wakimbizi huku machafuko na mapigano likiwa ni jambo la kawaida na la kila siku nchini humo na kuzusha hofu ya kuitumbukiza tena Burundi kwenye vita vya ndani vya mwaka 1993-2006.
Kumezuka wasiwasi kuwa watu wenye misimamo mikali wanazidi kuwa na ushawishi ndani ya chama tawala cha CNDD-FDD.
Mwanadiplomasia mmoja wa kigeni ambaye hakutaka kutajwa jina lake ameviambia vyombo vya habari kuwa kabla ya kuanza mgogoro nchini Burundi mrengo wenye misimamo mikali ndani ya chama hicho ulikuwa umetengwa, lakini ni wazi kwamba hivi sasa ndio wenye udhibiti wa nchi.../

0 maoni:
Chapisha Maoni