Jumapili, 27 Machi 2016

Idadi ya Waislamu yaongezeka Uganda, ya Wakatoliki yadidimia.



Idadi ya Waislamu yaongezeka Uganda, ya Wakatoliki yadidimia
Imearifiwa kuwa idadi ya watu wanaojiunga na dini tukufu ya Kiislamu nchini Uganda inazidi kuongezeka kwa kasi huku idadi ya wanaojiunga na Kanisa Katoliki ikizidi kupungua.
Matokeo ya sensa ya mwaka 2014 yaliyozinduliwa siku chache zilizopita na Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo yameonyesha kuwa, idadi ya Waislamu nchini humo imeongezeka hadi asilimia 13.7 mwaka 2014, kutoka asilimia 12.4 mwaka 2002. Aidha idadi ya wafuasi wa madhehebu ya Pentekosti imeongezeka kutoka asilimia 4.7 hadi asilimia 11.1.
Hata hivyo Msemaji wa Baraza Kuu la Waislamu nchini humo, Hajj Nsereko Mutumba amepuuzilia mbali takwimu hiyo ya asilimia 13.4 na kusisitiza kuwa, idadi ya Waislamu nchini humo ni asilimia 25.
Ripoti hiyo ya sensa ya mwaka 2014 ya Uganda kadhalika imeonyesha kupungua kwa idadi ya Wakatoliki nchini humo kutoka asilimia 41.6 mwaka 2002 hadi asilimia 39.3 mwaka juzi; sawa na ilivyopungua idadi ya wafuasi wa Kanisa la Kianglikana kwa asilimia 4. Hii ni kusema kuwa, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Wakatoliki laki 7 na 95 elfu na Waangalikana milioni moja na laki 6 ima waliingia katika dini tukufu ya Kiislamu au waligura na kujiunga na madhehebu ya Waprotestanti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Idadi ya Waislamu yaongezeka Uganda, ya Wakatoliki yadidimia. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top