Jumatatu, 6 Julai 2015

POPPE AMFUATA RIO SIMBA SC YALETA STRAIKA MBRAZIL HAKAMATIKI KAMA RONALDO, HANS POPPE AMFUATA RIO

KOCHA mpya wa Simba SC, Muingereza Dylan Kerr amewasilisha jina la mchezaji Mbrazil kwa uongozi wa Simba SC na kuwapa maelekezo alipo wamfuate kumleta nchini.
Na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe atapanda ndege Jumapili kwenda Rio de Jeneiro, Brazil kumfuata mshambuliaji huyo ambaye Kerr amewaambia anafunga kama Cristiano Ronaldo.
“Kocha ametuambia huyo mchezaji ni kama Ronaldo, hakamatiki kwa kufunga na kwa kuwa tunamuanini mwalimu wetu basi Jumapili napanda ndege kwenda kuzungumza na huyo mchezaji. Tukikubaliana, nitarejea naye,”amesema Kapteni wa zamani wa Jeshi ka Wananchi Tanzania (JWTZ
Hans Poppe kulia Jumapili atakwenda Brazil kufuata mchezaji

SImba SC ina nafasi mbili za wachezaji wa kigeni, baada ya sasa kuwa tayari ina wachezaji watano, ambao ni Waganda, beki Juuko Murushid, washambuliaji Hamisi Kiiza, Simon Sserunkuma na Emmanuel Okwi na Mrundi Laudit Mavugo. Tayari Simba SC ipo kwenye mkakati wa kusajili mchezaji mwingine wa Burundi. 
Wekundu wa Msimbazi wamepania kurejesha makali yao msimu ujao, baada ya misimu mitatu migumu iliyopita.
Na kwa kuanzia, Simba SC wameboresha benchi la Ufundi, safari hii wakiajiri makocha watatu wa kigeni chini ya Muingereza Dylan Kerr, Kocha wa mazoezi ya viungo, Mserbia Dusan Momcilovic, kocha wa makipa Mkenya, Abdul Iddi Salim wanaoungana na Kocha Msaidizi mzalendo Suleiman Abdallah Matola.
Simba SC inatarajiwa kuingia kambini kuanzia leo kuanza rasmi maandalizi ya msimu mpya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: POPPE AMFUATA RIO SIMBA SC YALETA STRAIKA MBRAZIL HAKAMATIKI KAMA RONALDO, HANS POPPE AMFUATA RIO Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top