Alhamisi, 30 Julai 2015

HII NI STORY YA KWELI NA INASIKITISHA SANA, KIGOGO AMTELEKEZA MKEWE MWENYE WATOTO 3 KISA KAISHIA DARASA LA SABA.

MDAI katika kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali Magreth Mwangu
mkazi wa Mkoani Singida dhidi ya Mkurugenzi wa Shule za sekondari za
St.Mathew na St Marks Thadei Mtembei amelalamikia kitendo cha Benki ya
CRDB kutoa taarifa zake za benki bila idhini yake wala ya mahakama.
Pia ameilalamikia mahakama ya Mwanzo Kizuiani inayosikiliza kesi hiyo
kwa kutumia Wakili wa kujitegemea licha ya kuwa mawakili hawaruhusiwi
katika mahakama ya Mwanzo.
Kesi hiyo inasikilizwa na hakimu Rajab Tamaambele.
Wakili huyo amekuwa akimwakilisha mdaiwa ambaye amekuwa hafiki
mahakamani tangu kesi hiyo ifunguliwe kwa kile kilichoelezwa wamepata
kibali kutoka kwa mwanasheria mkuu wa serikali kinachoruhusu kesi hiyo
kusikilizwa na wakili bila mdaiwa kuwepo.
Kwa mujibu wa Mwangu tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani hapo
mdaiwa amekuwa hafiki mahakamani na badala yake amekuwa akiwakilishwa
na mtoto wake,Peter Mtembei ambaye ni Wakili hali iliyofanya kesi hiyo
mpaka inaisha na kufungwa ushahidi mdaiwa akiwa hajasikiliza shahidi
hata mmoja.
Hata hivyo Mmiliki huyo wa St, Mathew juzi alifika mahakamani kufuatia
amri ya mahakama kufuatia malalamiko ya mdai aliyokuwa akitoa
mahakamani kutokana na Mtembei kushindwa kufika kwenye kesi hiyo tangu
ilipofunguliwa na  iliyomtaka afike mwenyewe mahakamani hapo na endapo
asingefika mahakama ingehamia nyumbani kwake.
Akitoa ushahidi wake, Mtembei alisema alifahamiana na Mwangu wakati
akiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.
Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa naye
watoto watatu.

Alisema mama huyo hana hadhi ya kuwa mke wake kwani ameishia darasa la
saba elimu ambayo ni ya chini sana.
“Huyu alikuwa ni mfanya usafi tu ni nesi msaidizi kazi yake ilikuwa ni
kufanya usafi na hata kufunga vidonda tu” alisema
Alisema duka hilo la dawa lilifungwa baada ya kuonekana aliyekuwa
analihudumia hana elimu.

Mtembei alisema mdai hana uhusiano na mali alizonazo kwani yeye ana
mke wake wa ndoa na huyo alikuwa ni mwanamke tu aliyezaa naye.
“Huyu ni mwanamke tu niliyezaa naye hana haki kwenye mali zangu” alisema
Alipohojiwa na mahakama kama alifunga ndoa na mdai alisema kuwa
hajawahi kufunga naye ndoa licha ya kutoa mahari ya ng’ombe watano.
“Nilimpelekea baba yake vindama vitano tu kama zawadi” alisema
Alisema hajawahi kufunga ndoa ya kimila na mdai kama inavyodaiwa na
mdai hana haki yoyote katika mali zake.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: HII NI STORY YA KWELI NA INASIKITISHA SANA, KIGOGO AMTELEKEZA MKEWE MWENYE WATOTO 3 KISA KAISHIA DARASA LA SABA. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top