Na sasa kinachosubiriwa na FS ni kumalizana na mchezaji juu ya maslahi binafsi- ili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania ahamie Ligi Kuu ya ABSA.
Mrisho Khalfan Ngassa aliyesajiliwa na Free State Mei mwaka huu kutoka Yanga SC, ndiye aliyemuunganishia Bocco dili la kujiunga na timu hiyo na akawapa viongozi wa timu hiyo namba za Bocco.
Mazungumzo ya awali baina ya FS na Bocco yamefanyika, lakini hawajakubaliana kwenye baadhi ya vipengele, ingawa inatarajiwa klabu hiyo itamrudia tena mchezaji huyo baada ya kufikia makubaliano na Azam.
John Bocco anatakiwa na Free State Stars ya Afrika Kusini |
FS imempa mshahara mzuri Bocco, mara mbili ya ule anaopata Azam FC kwa sasa, lakini mchezaji huyo anataka apewe na nyumba pia na baadhi ya vipengele virekebishwe.
Azam FC sasa iko radhi kabisa kumuacha Bocco aende kupata changamoto nyingine baada ya kuitumikia timu kwa zaidi ya miaka saba tangu haijapanda Ligi Kuu.
Awali, Azam FC ilikataa kumuuza Bocco Israel, Afrika Kusini na Algeria licha ya kufuzu majaribio huko- lakini sasa amepata zali la kuchukuliwa bila majaribio.
Bocco aliyezaliwa Agosti 5, mwaka 1989
alifanya majaribio kwa wiki kadhaa katika klabu ya Ligi Kuu Israel mwaka 2010 na baadaye Afrika Kusini katika klabu ya Supersport United.
John Bocco amewahi kufuzu Super Sport United ya Afrika Kusini, Azam FC ikakataa kumuuza |
Bocco alifuzu Supersport baada ya wiki mbili, lakini Azam FC ikagoma kumuuza kwa sababu ya dau dogo.
Mapema mwaka huu, klabu ya CRB Ain Fakroun ilitaka pia kumnunua Bocco ahamie Ligi Kuu ya Algeria ijulikanayo kama Professionnelle, lakini Azam FC wakakataa.
Juhudi za kumpata Bocco mwenyewe kuzungumzia ofa hiyo ya Afrika Kusini hazikufanikiwa kwa sababu yuko Uganda na timu ya taifa, Taifa Stars, ambayo inarejea leo.
0 maoni:
Chapisha Maoni