Mchezo ulikuwa ni mkali na wa kasi, timu zote zilijitahidi kutengeneza nafasi na kufanya mashambulizi kadhaa lakini milango yote miwili ilikuwa migumu kuruhusu nyavu kutikiswa na washambuliaji wa timu zote mbili.
Matias Fernandez, Arturo Vidal, Charles Arangui na Alexis walifunga mikwaju yao ya penati wakati wachezaji waliokosa penati kwa upande wa Argentina ni Gonzalo Higuain ambaye alipaisha juu wakati golikipa wa Chile Claudio Bravo alipangua mkwaju wa penati uliopigwa na Ever Banega huku Messi akiwa ni mchezaji pekee aliyefunga penati ya Argentina.
Ilibidi mikwaju ya penati iamue nani atanyanyua ndoo hiyo baada ya kushuhudia dakika 90 za mtanange huo zikimalizika bila timu yoyote kuzifumania nyavu za mpinzani wake. Zikaongezwa dakika 30 ambazo pia zilimalizika bila kumpata mbabe wa pambano hilo ndipo mikwaju ya penati ilipotumika kuamua nani ataondoka na mwali huyo aliyekuwa akigombewa na Mataifa ya 12 ya America Kusini.
Messi ameshashinda mataji yote kwenye ngazi klabu, lakini ameshindwa kutwaa taji lolote akiwa ametinga uzi wa Argentina.
0 maoni:
Chapisha Maoni