Timu ya kanda ya Zanzibar imefanikiwa kutwaa makombe mawili kwenye michuano ya UMMISSETA iliyomalizika jijini Mwanza na kurejea visiwani Zanzibar ikiwa kifua mbele kwa ushindi huo na kupokelewa na Mkurugenzi wa idara ya Michezo na Utamaduni Hassan Tawakal na kumkabidhi vikombe hivyo viwili walivyovipata.
Jumla ya wachezaji 116 kutoka kanda ya Zanzibar walishiriki kwenye michuano hiyo ambayo inahusisha michezo mbalimbali kwa vijana wa shule za sekondari Tanzania, walirejea visiwani Zanzibar wakiwa salama salimini baada ya safari ndefu ya kutoka Mwanza.
Zanzibar waliibuka washindi wa kwanza kwenye mchezo wa mpira wa mikono ‘handball’ kwa upande wa wavulana na kujinyakulia kombe, lakini pia walishika nafasi ya tatu kwenye mchezo wa wavu ‘volleyball’ kwa upande wa wavulana na kutwaa kikombe pia.
Tawakal amewapongeza wanafunzi wote walioshiriki michuano hiyo ya UMISSETA mwaka huu na kuwashukuru walimu na viongozi wote waliosafiri na timu na kuwa pamoja na vijana kwa siku zote hatimaye kurejea Zanzibar wakiwa salama.
0 maoni:
Chapisha Maoni