Jumatatu, 22 Juni 2015

Wadau wa soka watoa ya moyoni baada ya kipigo cha Stars, ingia hapa kujua walichokisema

Wadau mbalimbali walikuwa na maoni tofauti kufuatia kipigo cha goli 3-0 ilichopata timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ dhidi ya Uganda kwenye mchezo uliopigwa jana usiku kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar kuwania kufuzu kucheza mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
Kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelo yeye katika maoni yake aliomba apewe timu hiyo asaidiane na Charles Boniface Mkwasa pamoja na Morroco ili waiongoze na kuipeleka pale watanzania wanapotaka kuiona timu hiyo. Lakini si Julio pekee ambaye alipata fursa ya kutoa maoni baada ya mchezo huo kumalizika, wadau wengine pia walitoa yao ya moyoni.
Kila mmoja amekuwa na maoni tofauti, wengi wakionesha kuchukizwa na matokeo ya Stars ya hivi karibuni pamoja na kuchoshwa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mart Nooij pamoja na benchi zima la ufundi lililokuwa linakiongoza kikosi hicho.
Lakini wapo waliokuwa wakisema bado kocha anahitaji kupewa muda wa kukaa na wachezaji ili kuendelea kukiboresha kikosi hicho wakidai hata akija kocha mwingine bado tatizo litaendelea kuwa lilelile hivyo ni vizuri kutoa muda mrefu kwa kocha ili aendelee kufanya mabadiliko kulingana na mahitaji ya timu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Wadau wa soka watoa ya moyoni baada ya kipigo cha Stars, ingia hapa kujua walichokisema Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top