Jumatatu, 22 Juni 2015

Julio ajipigia debe apewe Stars, autaja mzizi wa ‘fitna’ unaoitafuna…

Kufuatia uamuzi wa TFF kulitimua benchi la ufundi la timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameonesha nia ya kutaka apewe majukumu ya kukifundisha kikosi cha timu ya Taifa huku akitaka kupewa ushirikiano kama wanaopewa makocha wa kigeni pindi wanapopewa kazi ya kuifundisha timu.
 Julio amesema anataka apewe kikosi hicho akishirikiana na Morocco pamoja na Charles Boniface Mkwasa ili waweze kukivusha na kukifikisha kwenye michuano ya kombe la dunia.
“Kama kweli mnataka kuamini wazawa basi muwape ‘support’ kama mnavyofanya kwa wazungu, mi naamini timu hii kama mnatengeneza ‘combination’ sio kama najipigia debe, mimi mpalestina najisifia mwenyewe lakini mnipe mimi, Morocco na Charles Boniface Mkwasa hii nchi tutaivusha na tutakupelekeni ‘world cup’”, amesema Julio.
“Unapotaka kukodi tax kwenda mahala popote, unafungua mlango unaingia na kuondoka lakini kama huna pesa itabidi utie shingo umwambie dereva, ebwana hapa mpaka pale ni bei gani ili mpatane. Sasa mpira hauna ‘short curt’, mpira unamipango mingi ambayo tunatakiwa tufanye. Kwahiyo tatizo kubwa la mfumo tunaosema unatakiwa tuwe asilimia mia moja fiti, wachezaji wetu ‘fitness level’ yao iko chini ‘that’s why’ umeona ‘second half’ waganda wametushambulia na wangeweza kutufunga hata goli nyingi”, amefafanua Julio.
“Walikuja kwa kulinda kwamba wao wasifungwe kwasababu wanacheza ‘away’ lakini walivyopata goli moja ‘waka-gain confidence’, walipokuja second half wakaona kumbe tunaweza, wakapata goli la pili na la tatu na kama muda ungeongezeka basi nafikiri aibu zaidi ingetukuta. Kwahiyo lazima wachezaji unaowachagua ujue wanakwenda kucheza na watu wa aina gani na unachowafundisha kina swihi?”, Julio alihoji.
“Kwasababu hata sisi waislam tumeagizwa kuswali swala tano lakini bado kuna mgogoro, wengine wanaswali wengine hawaswali ingawa Mungu anataka tuswali muda wote. Sasa na wewe unatakla kuwachezeha wachezaji 3-5-2, je fitness level yao iko sawa? Kwasababu wanatakiwa hawa ma-fullbacks wanaitwa ma-wingbacks muda wote wakapige krosi kama vile akina Roberto Carlos”, ameeleza.
“Lakini sisi mabeki wetu wanakuja kuzuia, kushambulia hawaendi sasa hiyo 3-5-2 gani? Kwahiyo hii sababu ya kufungwa tumeitengeneza wenyewe tusilalamike, tumevuna tulichopanda”, alimaliza Julio
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Julio ajipigia debe apewe Stars, autaja mzizi wa ‘fitna’ unaoitafuna… Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top