Jumatatu, 22 Juni 2015

BRAZIL BILA NEYMAR YACHINJA 2-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI COPA AMERICA

BRAZIL imefanikiwa kwenda Robo Fainali Copa America kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Venezuela usiku wa kuamkia leo nchini Chile inapoendelea michuano hiyo. 
Ikicheza bila ya nyota tegemeo lake, Neymar aliyefungiwa mechi nne kwa utovu wa nidhamu aliouonyesha katika mchezo dhidi ya Colombia, Brazil ilipata mabao yake kupitia kwa Thiago Silva dakika ya tisa na Roberto Firmino dakika ya 51.
Fedor ndiye mfungaji wa bao pekee la Venezuela, aliyemtungua kipa Jefferson zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika na sasa Brazil itakutana na Paraguay katika Robo Fainali Jumamosi.
Kikosi cha Brazil kilikuwa; Jefferson, Alves, Silva, Miranda, Filipe Luis, Fernandinho, Elias, Willian, Coutinho/Tardelli dk67, Firmino/Luiz dk67 na Robinho/Marquinhos dk76.
Venezuela: Baroja, Rosales, Tunez, Vizcarrondo, Chichero, Rincon, Vargas/Gonzalez, Seijas/Martinez dk46, Guerra/Fedor dk72, Arango na Rondon.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Colombia imelazimishwa sare ya 0-0 na Peru, huku mshambuliaji Radamel Falcao akitolewa uwanjani dakika ya 65 baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya ukuta wa Peru.
Sare hiyo inazifanya timu zote hizo zimalize mechi za Kundi C na pointi nne kila moja na Peru inakwenda Robo Fainali moja kwa moja kama mshindi wa pili nyuma ya Brazil.
Sare hiyo pia inaitupa nje ya michuano hiyo Ecuador iliyokuwa Kundi A, ambayo imemaliza na wastani mbaya zaidi kati ya washindi wa tatu wa makundi yote. Colombia sasa itamenyana na Argentina katika Robo Fainali.
Silva akiwa amezungukwa na wachezaji wenzake wa Brazil kupongezwa Uwanja wa  Estadio Monumental baada ya kufunga bao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: BRAZIL BILA NEYMAR YACHINJA 2-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI COPA AMERICA Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top