Jumanne, 30 Juni 2015

CHILE WATINGA FAINALI COPA AMERICA, MCHEZAJI PERU ALIMWA 'UMEME' MAPEMA KABISA

 Wenyeji Chile wametinga hatua ya fainali ya Copa America baada ya kuifunga timu pungufu ya Peru magoli 2-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa usiku wa kuamkia leo mjini Santiago.
 Eduardo Vargas ameifungia Chile magoli mawili katika dakika ya 42' na 64', lakini dakika ya 60' Mlinzi Gary Medel alijifunga bao na kuwapa angalau ahueni Peru.
Mapema dakika 20' Mwamuzi wa mechi, Jorge Argote alimuonesha kadi nyekundu (Umeme) Carlos Zambrano kwa kosa la kumkanyaga mgongoni kiungo wa Chile,Charles Aranguiz.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: CHILE WATINGA FAINALI COPA AMERICA, MCHEZAJI PERU ALIMWA 'UMEME' MAPEMA KABISA Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top