Jumanne, 30 Juni 2015

COPA AMERICA: WENYEJI CHILE WATINGA FAINALI, EDUARDO VARGAS SHUJAA!

Bao mbili za Mchezaji wa zamani wa QPR ambae sasa yupo Napoli huko Italy, Eduardo Vargas, zimewafikisha Wenyeji Chile Fainali yao ya kwanza ya Copa America baada ya Miaka 28 walipoifunga Mtu 10 Peru 2-1 hapo Jana huko Estadio Nacional de Chile Jijini Santiago.
Chile, ambao hawajawahi kutwaa Copa America katika Miaka 99 ya Historia yake, wamebahatika kwa Kiungo wao Arturo Vidal kubaki Uwanjani baada ya kuinua mkono kumpiga Carlos Zambrano lakini Refa hakuwa na huruma kwa  Zambrano alieambua Kadi Nyekundu katika Dakika ya 20 tu baada ya kumchezea Rafu Charles Aranguiz.
Bao za Vargas zilifungwa Dakika za 42 na 64 na Peru kupata Bao lao Dakika ya 60 baada Gary Medel kujifunga mwenyewe.
Kwenye Fainali Chile watacheza na Mshindi kati ya Argentina na Paraguay wanaokutana Leo Usiku katika Nusu Fainali nyingine.
VIKOSI:
Chile (Mfumo 4-3-1-2): Bravo; Isla, Medel, Rojas, Albornoz; Vidal, Diaz, Aranguiz; Valdivia; E. Vargas, Alexis.
Akiba: Mena, Silva, Fuenzalida, Pinilla, Garces, Fernandez, Beausejour, D. Pizarro, Gutierrez, Henriquez, Herrera.
Peru (Mfumo 4-2-3-1): Gallese; Advincula, Zambrano, Ascues, J. Vargas; Lobaton, Ballon; Farfan, Cueva, Carrillo; Guerrero.
Akiba: Cespedes, Riojas, Requena, Hurtado, Reyna, Penny, Retamoso, C. Pizarro, Ramos, Yotun, Sanchez, Libman.
REFA: Jose Ramon Argote Vega [Venezuela]
Match # 23
1:0Half-time
COPA AMERICA
RATIBA/MATOKEO:
ROBO FAINALI
Jumatano Juni 24
Chile 1 Uruguay 0
Alhamisi Juni 25
Bolivia 1 Peru 3
Ijumaa Juni 26
Argentina 0 Colombia 0 (Penati-Argentina washindi 5-4)
Jumamosi Juni 27
Brazil 1 Paraguay 1 ( Penati-Paraguay washindi 4-3 )
NUSU FAINALI
Jumatatu Juni 29
Chile 2 Peru 1
Jumanne Juni 30
Argentina v Paraguay (Saa 8 na Nusu Usiku)
MSHINDI WA 3
Ijumaa Julai 3
(Saa 8 na Nusu Usiku)
Peru v Argentina/Praguay
FAINALI
Jumamosi Julai 4
(Saa 5 Usiku)
Chile v Argentina/Praguay
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: COPA AMERICA: WENYEJI CHILE WATINGA FAINALI, EDUARDO VARGAS SHUJAA! Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top