Sekta ya Mifugo ina nafasi kubwa
katika kujenga uchumi imara wa Taifa, kuongeza kipato kwa Watanzania
wanaotegemea mifugo, na kutoa fursa za ajira sanjari na kuhifadhi rasilimali za
Taifa.
![]() |
![]() |
kwa masilia zadi no:0752-2840777 |
Yapo
mabadiliko chanya katika Sekta ya Mifugo nchini ambayo yameanza kujionyesha,hususan
katika uzalishaji na uuzaji wa mifugo na ma zao yake nje ya nchi,utoaji wa
huduma na upatikanaji wa pembejeo za mifugo na hawa mingoni mwa viongzi wa Bina Foundation Singida.
Mkazo
wa Bina Foundation utaendelea kuwekwa
katika kugharamia huduma za ufugaji zinazoh itajika kukuza sekta kwa ufanisi.
Huduma hizo ni pamoja na miundombinu ya vijijini, utafiti huduma za ugani, uzuiaji
magonjwa ya mlipuko na udhibiti wa wadudu waenezao magonjwa ya mifugo.
Aidha, Bw.
Piter amiomba Serikali kuhamasisha
wafugaji na wadau wengine kuchangia gharama
za utoaji wa huduma kama vile ujenzi wa malambo na majosho nchini.
(TPFC)Ni Jukwaa la Jamii ya Wafugaji Tanzania (TPCF), juzi lilizindua rasimu ya sera ya ufugaji wa asili nchini, ili iweze kujadilidiwa na wafugaji na baadaye ipelekwe serikalini, ili kusaidia kuandaliwa sera rasmi ya ufugaji wa asili nchini.
![]() |
wanafunzi kutoka mkoa Dodoma baada ya kupokea msada kutoka kwa wakurugenzi wa Bina Foundation. |
Mratibu wa jukwaa hilo, Joseph Parsambei aliwasilisha rasimu ya sera hiyo juzi katika kongamano la jukwaa la wafugaji, lililofanyika Arusha na kuhudhuriwa na wawakilishi wa wafugaji kutoka mikoa ya wafugaji.
![]() |
Mganga alifanikisha kumzalisha Ngombe Kwa upasuaji katika sehemu ya ufugaji Ndani ya Bina Foundation. |
![]() |
Nguruwe zipo kwa wingi katika mradi wa Bina Foundation Singida.kwa masilia zadi no:0752-2840777 |
![]() |
kwa masilia zadi no:0752-2840777 |
Bw. Peter Bina bada ya kukutana na waataalam na hapa anaelezea Homa ya Bonde la Ufa (HBU) (Rift valley fever) ni ugonjwa wa
kirusi unaojitokeza kwa dharula ukishambulia hasa wanyama wanaocheua
(ngo'mbe, mbuzi, kondoo), lakini wanyama wengine pia hupata kama punda, ngamia na wanyama pori
mfano nyati, nyumbu na swala . Mwanadamu pia hupata ugojwa huu kutoka kwa
wanyama walio na ugonjwa huu kwa kula nyama isiyopimwa na kupikwa vizuri au kwa
kushika mazao ya wanyama wenye ugonjwa . Ugonjwa unasababishwa na virusi vya
homa ya bonde la ufa homa (VHBU) vinavyo sambazwa na mbu aina ya Aedes. HBU
huleta madhara makubwa sana kiuchumi na kijamii pale unapotokea na hasa hatua
za makusudi za kuzuia kuenea kwake zisipo chukuliwa. Kuwepo kwa wanyama wanao
tupa mimba kwa wingi kati ya kondoo, mbuzi, ng'ombe na ngamia na vifo vya
wanyama wadondo (watoto wa mbuzi, kondoo, na ndama) kwa karibu asilimia mia
moja na uwepo wa dalili zinazofanana na mafua ya ndege ni viashilia tosha vya
kuwepo kwa HBU. Historia ya kuwepo kwa mvua nyingi kiasi cha kutengeneza
mafuriko pamoja na ongezeko la mbu wanaoeneza ugonjwa huu ni kiashiria cha
kuanzia kufanya uchunguzi wa kina ili hatua mahususi ziweze kuchukuliwa.
kuku wa kienyeji wanapatika kwa wingi katika mradi wa Bina Foundation Singida |
Lakini
miaka mitatu iliyopita ulipiga hodi hapa nchini na kuua watu katika mikoa
ambayo Bonde la Ufa linapita hasa maeneo ya Arusha na Manyara, Kanda ya Kaskazini
mwa Tanzania.
Ugonjwa
wa homa ya bonde la ufa ulioonekana kwa mara ya kwanza Kenya, matukio yake
makubwa yameonekana katika nchi nyingi za Bara la Afrika, ikiwa ni pamoja na
Misri, Sudan, Somalia, Kenya, Msumbiji, Nigeria, Senegal, Tanzania, Uganda,
Zambia, Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini.
Nchi
ya Misri ilikumbwa na ugonjwa huu mwaka 1977 na 1978 ambapo watu wapatao 18,000
waliugua na 598 walikufa. Nchi ambazo taarifa zilitolewa za matukio ya ugonjwa
huu nje ya Bara la Afrika ni pamoja na Yemen na Saudi Arabia.
Kwa
hapa Tanzania ugonjwa huu ulionekana mwaka 1979 na 1998 katika mikoa ya Mara,
Arusha na Kilimanjaro ambapo ng’ombe, mbuzi, kondoo na ngamia waliathirika.
HBU
ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vijulikanvyo kama virusi vya homa ya bonde
la ufa (VHBU) vilivyopo kwenye familia ya virusi ya Bunya (Bunyaviridae). VHBU
vimekuepo tangu zamani sana na viligunduliwa kitaalamu kwa mara ya kwanza
nchini Kenya mnamo mwaka 1931 katika bonde la ufa (Rift Vlley), kiini cha jina
la ugonjwa. Vinasaba vya kirusi hiki ni vya aina ya RNA na ina vipingili vitatu
ambavyo husaidia kirusi huyu kutengeneza aina nyingine ya kirusi yuleyule na
kumfanya asishambuliwe na kinga ya mwili ya mnyama.
![]() |
Kwale (pia kware)
ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia ya Phasianidae.
Spishi nne za Francolinus ambazo zina
ngozi kichele yenye rangi kali kooni na pande zote za macho huitwa kereng'ende
pia. Rangi ya kwale ni kahawia au kijivu na wana michirizi au madoa. Mara
nyingi miguu yao ni myekundu au rangi ya manjano na koo lao ni jekundu, jeupe,
jeusi au rangi ya manjano. Hujificha kwa kawaida lakini sauti yao husikika mara
kwa mara. Chakula chao ni mbegu, wadudu
na nyungunyungu.
Hutaga mayai matatu hadi kumi ardhini pengine juu ya manyasi makavu.
![]() |
Kwale (ndege)kwa masilia zadi no:0752-2840777
|
![]() |
Mayai ni bidhaa hafifu na inayoharibika kwa
haraka. Hivyo, ni lazima ishikwe kwa uangalifu na kutunzwa vizuri baada ya
kutagwa ili yasivunjike au kuharibika. Watu wengi wanaonunua mayai kutoka
dukani watatambua mara moja kuwa mayai hayo yamevunjika au yameoza. Tatizo hili
linaweza kutokana na utunzaji na uhifadhi wakati mayai bado yakiwa kwa mfugaji.
Ili kupunguza hasara, ni lazima mfugaji
ahakikishe kuwa mayai yanafika sokoni yakiwa bado mapya na salama. Utunzaji
sahihi wa mayai huyafanya yaepukane na madhara yanayoweza kutokana na viumbe
wadogo wadogo kama vile bakteria, wanyama walao mayai, upotevu wa unyevu, au
joto wakati wa uhifadhi na kusafirisha kwenda sokoni, jambo linaloweza
kuyafanya yavunjike. Mayai kama ilivyo kwa viumbe hai wengine yanahitaji
kupumua. Trei za kuhifadhia mayai ziwekwe kwenye sehemu yenye hewa
inayozunguka, hasa hewa ya oxyjeni.
Trei zote za kuhifadhia mayai ni lazima ziwekwe
katika hali ya usafi, zisiwe na harufu ili kuepuka kufishwa au kusababisha hali
yoyote inayoweza kusababisha uharibifu. Mayai ni lazima pia yakingwe dhidi ya
joto kali pamoja na unyevu.
![]() |
Jinsi ya kutunza vifaranga kwa masilia zadi no:0752-2840777
|
Mayai yanaweza kuharibika kwa haraka kutokana na
joto kali. Labda yahifadhiwe kwenye jotoridi la chini, vinginevyo mfugaji
atapoteza idadi kubwa ya mayai kabla hayajafika sokoni. Ni lazima kuhakikisha
kuwa mayai yanahifadhiwa sehemu yenye ubaridi, ambayo siyo kavu sana, vinginevyo
yatapoteza unyevu kwa haraka endapo yatawekwa sehemu kavu. Hali ya mahali pa
kuhifadhia inategemea na siku ambazo mfugaji anahitaji kuhifadhi mayai.
Wafugaji wenye uzoefu wamekuwa na uwezo wa
kuhifadhi mayai kwa kipindi cha miezi 6-7 kwa kutumia jokofu. Wafugaji wadogo
pia wanaweza kuhifadhi mayai kwa siku kadhaa mpaka watakapopata mayai kwa ajili
ya kuhatamiwa. Kamwe usihifadhi mayai unayokusudia kutumia kwa ajili ya
kuhatamiwa kwenye jokofu.
Uhifadhi wa mayai kwa ajili ya kuhatamia
Wafugaji wadogo hutumia njia ya kiasili
kuhatamisha na kuangua mayai. Hii ni njia ya kutumia kuku au ndege mwingine
ambaye hupewa mayai na kuyahatamia hadi kuanguliwa. Kuku wa kienyeji ni wazuri
sana wanapotumiwa kwa ajili ya uzalishaji wa vifaranga. Hata hivyo kwa uzalishaji
mzuri ni lazima mfugaji ahakikishe kuwa kuku anapewa mayai yenye uwezekano
mkubwa wa kuanguliwa.
Mbinu moja wapo ambayo mfugaji anaweza kuitumia
kutambua mayai yenye uwezekano mkubwa wa kuanguliwa ni kwa kumulika kwa kutumia
mshumaa. Mayai yanaweza kuwekwa kwenye mwanga mkali ambao utakuwezesha kuona
ndani ya yai. Kifaa rahisi cha kumulika mayai kinaweza kutengenezwa kutokana na
kuweka balbu ndani ya boksi dogo. Unakata tundu dogo kuruhusu mwanga. Hakikisha
linakuwa na ukubwa wa kuweza kuruhusu yai kukaa juu yake.
Shika yai kwa kulisimamisha kwa kutumia vidole
vyako viwili, kasha liweke kwenye mwanga wa tochi au balbu. Zoezi hili linakupa
uhakika kuwa mayai yenye uwezekano wa kuanguliwa ndiyo pekee yanayochaguliwa.
Tengeneza sehemu ya kuhatamia mayai
Mfugaji anaweza kuboresha uzalishaji wa kuku wa
kienyeji kwa kuwajengea tabia ya kuhatamia mayai. Kuku wa kienyeji wakiwa
wamelishwa vizuri, wanaweza kuhatamia kati ya mayai 10-14 kwenye mzunguko
mmoja. Baada ya kuangua, mfugaji amruhusu kuku kukaa na vifaranga walau kwa
wiki moja. Baada ya hapo vifaranga wanaweza kutengwa.
Kuku wakiwa bado katika hali ya kuhatamia,
anaweza kupewa mayai ya bandia ambayo yanaweza kutengenezwa kutokana na sabuni,
huku kuku wengine wakiwa wamehatamia mayai halisi ya kutosha. Mayai bandia
yanaweza kuondolewa na kuku kuwekewa mayai halisi aendelee kuhatamia mpaka
yatakapoanguliwa.
Kuku wanaohatamia ni lazima wapatiwe chakula na
maji ya kutosha. Kuku ambao hawahitajiki kwa ajili ya kuendelea kutotoa,
wanyang’anywe vifaranga na kuachiliwa walipo kuku wengine. Ni vizuri kuweka
alama kila yai kuonesha ni tarehe gani lilitagwa, hii itamsaidia mfugaji
kutokuchanganya mayai ya zamani na mayai mapya. Badala yake, mfugaji anaweza
kuwatenga kuku ambao amewaandaa
kwa ajili ya kutotoa na wale ambao ni kwa ajili
ya kutaga tu ili asichanganye mayai yake.
0 maoni:
Chapisha Maoni