Jumapili, 8 Februari 2015

Kamu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini, Bw. Joseph Sabore amekiri kupokea taarifa kutoka kwa watumishi wa zahanati ya Mvae iliyopo katika tarafa ya Ilongero kuwa wanafanyiwa vitendo vya kishirikina nyakati za usiku.



Bw. Sabore ameiambia Standard Radio kupitia kipindi cha Zinduka kuwa, watumoishi hao wanapaswa kuvuta subira, ili mkutano wa hadhara uitishwe na kujadili suala hilo kwa pamoja na wakazi wa eneo hilo.

Hata hivyo, amesema kuwa serikali haiamini mambo ya kishirikina na kuwaomba watumishi hao kuendelea kufanya kazi wakati malalamiko yao yanatafutiwa ufumbuzi.

Aidha amesema hii sima mara ya kwanza kutokea kwa malalamiko kama hayo kutoka kwa watumishi wa serikali walio katika maeneo mbali mbali katika halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Kamu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini, Bw. Joseph Sabore amekiri kupokea taarifa kutoka kwa watumishi wa zahanati ya Mvae iliyopo katika tarafa ya Ilongero kuwa wanafanyiwa vitendo vya kishirikina nyakati za usiku. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top