Jumapili, 8 Februari 2015

Habari kutoka Mkoani Singida



MANYONI


Serikali kuu inatarajia kuipatia wilaya ya Manyoni mkoani Singida zaidi ya shilingi milioni mia nane kugharamia matengenezo ya barabara mbalimbali katika mwaka wa fedha wa 2015/2016.

Hayo yamesemwa na waziri wa ujenzi Dk.John Magufuli,wakati akizungumza na wakazi wa tarafa ya Itigi wilaya ya Manyoni muda mfupi baada ya kumaliza kukagua barabara yenye urefu wa kilometa 89.3 ya Manyoni-Itigi-Chaya mpakani na mkoa wa Tabora, inayojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya Sinho Hydro.

Amesema fedha hizo zitakazotoka kwenye mfuko wa barabara, zitatumika kugharamia matengenezo ya barabara, madaraja na barabara za lami kwenye baadhi ya miji ya wilaya ya Manyoni.

Kuhusu barabara ya kuanzia kijiji cha Mkiwa – Itigi hadi Rungwa mpakani na mkoa wa Mbeya,waziri huyo amesema kazi ya upembuzi yakinifu ili barabara hiyo iweze kujengwa kwa kiwango cha lami, imekamilika na kwa sasa bado hatua mbalimbali zinachukuliwa kabla ya kutafuta mkandarasi wa kuijenga.

Dk. Magufuli amesema upatikanaji wa fedha za ujenzi wa barabara, kwa kiasi kikubwa umechangiwa na mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, Bw. John Lwanji.




IKUNGI
Kijana mmoja  mkazi wa kitongoji cha Iporyo – kijiji cha Msungua kata ya
Sepuka wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Bw. Shabani Athuman Ilolo (23) amenusurika kufa baada ya kufumaniwa na kupigwa, kuchomwa na kitu chenye ncha kali mbavuni na mabegani.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Iporyo Bw. Saidi Athumani Ng’imba amesema  kuwa kijana huyo alikuwa na mazoea ya kwenda kwenye nyumba hiyo usiku akidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo, wakati mume wake asipokuwepo.

Habari zinasema mume wake alikuwa amesafiri kwenda Geita tangu mwezi
Oktoba 2014 na siku ya tukio alikuwa amerudi nyumbani kwake usiku 3 na alipofika kwake alikuta mlango umefungwa lakini viatu vya mwanaume huyo vilikuwa nje.  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Bw. Thobias Sedoyeka amethibitisha
kuwepo kwa tukio hilo ambapo mume wa mwanamke huyo anaisaidia polisi kutoa maelezo na baada ya hapo taratibu zingine zitafuata.
Hata hivyo ameonya watu kutokujichukulia sheria mikononi, kwani  ni kinyume cha sheria .




* Muungano wa mtandao wa mashirika yanayopinga  ukeketaji  wanawake umeeleza kushtushwa na ongezeko la idadi ya ukeketaji watoto wachanga  unaofanywa  kwa mbinu na wahusika tofauti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Habari kutoka Mkoani Singida Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top