Boko Haram lashambulia nchi Jirani.
Kundi la wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria limeshambulia mji mmoja nchini Niger kwa mara ya kwanza, mashahidi wamesema.
Shambulizi hilo la mji uliopo mpakani wa Bosso ni la pili la kundi hilo katika nchi jirani katika siku nyingi.Wapiganaji wake waliripoti kuwaua takriban watu 70 katika shambulizi la mji wa Fotokol nchini Cameroon siku ya alhamisi.
Uvamizi wa kundi hilo umesababisha mauaji ya maelfu ya watu huku wengine zaidi ya millioni wakiwachwa bila makao katika kipindi cha miezi sita iliopita.
Wapiganaji hao wanadhibiti eneo kubwa la ardhi kazkazini mashariki mwa Nigeria.
Mwandishi wa BBC katika eneo hilo amesema Boko Haram walishambulia mji wa Bosso wakitumia silaha kali,na kuwalazimu wakaazi kutoroka na kujificha ndani ya nyumba zao.
Wanajeshi wa Niger na Chad ambao wana kambi yao mjini Bosso,walikabiliana na Wapiganaji hao wakijaribu kuwafurusha.
0 maoni:
Chapisha Maoni