Waasi wa Shia wametangaza kutwaa
uongozi wa kisiasa nchini Yemen, kuvunjilia mbali bunge, kumwondoa rais
na nafasi hiyo kuchukuliwa na baraza la urais.
Wahouthi hao
walitangaza hayo katika mkutano wa siasa walipokuwa najeshi na wakuu wa
makabila katika ikulu ya nchi katika mji mkuu, Sanaa.Tukio hilo linajiri baada ya mazungumzo yaliyoongozwa na umoja wa mataifa ya kukomesha mzozo wa Yemen kusambaratika.
Rais Mansour Abdrabbuh Hadi na serikali yake walijiuzulu mwezi uliopita baada ya waasi hao kuthibiti mji wa Sanaa.
0 maoni:
Chapisha Maoni