Ngome nyengine ya Al-Shabaab yaanguka
Mji wa bandari wa Barawe nchini
Somalia ambao ulikuwa umetajwa kuwa ngome ya mwisho ya kundi la Al
shabaab umethibitiwa na vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa
muungano wa Afrika.
Mji wa Barawe ulio umbali wa kilomita 200
Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa Mogadishu umekuwa chini ya udhibiti wa
wanagambo wa Al Shabaab kwa miaka sita.Muungano wa Afrika unasema kuwa wanamgambo wamekuwa wakiutumia mji huo kama kituo cha kupanga mashambulizi dhidi ya mji mkuu Mogadishu.
Wapiganaji wa Al-Shabaab walianza kuondoka katika mji huo siku chache zilizopita.
0 maoni:
Chapisha Maoni