MSANII MKONGWE ALI CHOKI AFIWA NA MKEWE
Mkurugenzi
wa Extra Bongo, Ali Choki. MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, Ali
Choki amepata pigo la kuondokewa na mke wake, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’
baada ya kuugua kwa muda mrefu Usiku wa kuamkia leo.Akizungumza kwa
masikitiko Ali Choki alisema mke wake ameugua kwa muda wa miezi tisa
akiwa anasumbuliwa na mguu ambapo alitibiwa nchini India ikashindikana
akarudishwa nyumbani mpaka mauti yalipomfika usiku wa kuamkia Jumamosi
iliyopita.
“Ukweli
nimeumia kwani mke wangu ndiye aliyekuwa mshauri wangu mkuu na ndiye
kila kitu kwangu alikuwa akinisapoti kwenye kazi yangu ya muziki lakini
ndiyo hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,”alisema Ali Choki.
Aidha
Choki alisema mipango ya mazishi ilifanyika nyumbani kwao Tuangoma
Kigamboni na mazishi ya mkewe yatafanyika siku ya kesho saa kumi jioni
katika makaburi ya Chang’ombe Madukamawili.
0 maoni:
Chapisha Maoni