AIBU KUBWA: MKE, MUME WAVUANA NGUO LIVE WAKIZICHAPA HADHARANI..WAFUNGA MTAA KWA SINEMA YA BURE!
Hii
ni aibu kubwa! Njemba mmoja aliyefahamika kwa jina la Zeno na mkewe
Mwajuma Mtata, wakazi wa mtaa Mrefu, Kigogo-Luhanga jijini Dar wamenaswa
wakiangusha bonge la timbwili barabarani na kusababisha umati wa watu
kujikusanya eneo hilo kujionea ‘sinema’ ya bure.Timbwili zito likianza
kati ya njemba mmoja anayefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma
Mtata. Tukio hilo lililofananishwa na muvi ya kivita lilitokea usiku wa
Jumanne iliyopita ambapo chanzo kimedaiwa kuwa ni mwanamke huyo
kutelekeza jikoni kitoweo cha maini ya mbuzi na kwenda baa kupata
kilaji.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio, Zeno alirudi nyumbani mida ya
jioni mkononi akiwa na kifurushi chenye maini ya mbuzi pamoja na
mazagazaga mengine zikiwemo ndimu, tangawizi, pilipili hoho, nyanya na
vitunguu kupokelewa na ‘mai waifu’ wake huyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni