MKATABA WA MOSOTI, SIMBA UMEVUNJWA – FIFA
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Wakati
uongozi wa Simba ukidai kuwa bado una mkataba na beki Mkenya Donald
Mosoti, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeitaka klabu hiyo
kumlipa fidia beki kwa kuwa mkataba wake umevunjwa.
Katibu
Mkuu wa Simba, Stephen Ally alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari
nchini jana akisema kuwa Mosoti bado ni mchezaji wao halali kwa vile
mkataba kati yao na mchezaji huyo badi haujavunjwa.
Klabu
hiyo kongwe nchini, iliamua kumwacha beki huyo dakika za mwisho za
usajili msimu huu ili kumsajili Emmanuel Okwi aliyevunja mkataba wake na
Yanga huku mwanasheria wa Mosoti, Felix Majani akidai kuwa uamuzi huo
ulifanywa bila kumshirikisha mteja wake.
Mwanasheria
huyo anayeishi Ureno amekaririwa na mtandao wa Futaa.com wa Kenya leo
asubuhi akieleza kuwa ilibidi kuvunja mkataba wa Mosoti na Simba kwanza
kabla ya kulifikisha mbele ya FIFA kwa kuwa Simba walikuwa bado wanadai
kwamba Mosoti ni mchezaji wao na walitaka aidha wamuuze au kumtoa kwa
mkopo.
Majani
amesema kuwa mteja wake anataka Simba imlipe fidia kwa kuvunja mkataba
wake ilhali alikuwa bado ana muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu
kuitimkia klabu hiyo ya Msimbazi. “Kimsingi Mosoti anataka fidia na
ameomba adhabu za kisoka zichukuliwe dhidi ya Simba, kwa kufungiwa
kusajili wachezaji kwa misimu miwili ijayo ya usajili na tayari FIFA
imeshauandikia barua uongozi wa Simba kuukumbusha juu ya kesi hii,”
amesema Majani.
Beki wa
kushoto Mkenya John Njoroge alikumbana na tatizo kama la Mosoti dhidi ya
Yanga 2011 sought baada ya klabu hiyo ya Jangwani kuvunja mkataba bila
kumshirikisha na baadaye mchezaji huyo alinufaika kwa kupata fidia ya
Sh. milioni moja za Kenya, shukrani kwa maamuzi ya FIFA.
0 maoni:
Chapisha Maoni