Mbeya City yavuna saba mchangani
KAMA ilikuwa ni Ligi tungesema Mbeya City imeambulia pointi saba
baada ya kushinda mechi mbili za kirafiki na kutoa sare moja. Kikosi
hicho cha Juma Mwambusi juzi kilipata wakati mgumu mbele ya Shinyanga
United ya hapa na kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi iliyochezwa
kwenye Uwanja wa Majimoto lakini straika, Paul Nonga akatoa onyo.
Katika mechi mbili za awali kwenye ziara hiyo dhidi ya Mazwi FC ya Sumbawanga na Makanyagio FC ya Katavi, Mbeya City ilichapa mtu mabao 3-0 kila mechi.
Vijana wa Majimoto walionekana kuikamia Mbeya City juzi kwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara kwenye lango lao huku wakiweka ulinzi imara kuhakikisha washambuliaji wa City hawapiti kiurahisi.
Bao la Shinyanga United lilifungwa na Kisiga
Yusuph huku la Mbeya City likikung’utwa na Themi Felix. Kocha Msaidizi
wa Shinyanga United, Celina Ernest, alisema kuwa hakutarajia kuona
vijana wake wakilazimisha sare hiyo.
Paul Nonga ambaye ni tegemeo kwa Mbeya City alisema matokeo hayo ni changamoto kwao na kwamba walikuwa wakijifurahisha tu na kujua mashabiki wao.
Msimu uliopita kulikuwa na hofu ya ugeni kwenye
Ligi Kuu lakini msimu ujao watanitaka ubaya,” alisema Nonga na
kusisitiza ana imani kubwa na timu hiyo msimu ujao.
0 maoni:
Chapisha Maoni