Mkazi mmoja
wa kijiji cha Mloe, mkoani Kilimanjaro aliyejulikana kwa jina moja la
Agustin (47) anadaiwa kumbaka na kumpa mimba binamu yake mwenye umri wa
miaka 16 (jina linahifadhiwa) aliyekuwa kidato cha pili katika shule ya
sekondari ya Okaoni Septemba mwaka jana huko Dakau, Kibosho.
Akielezea tukio hilo, msichana huyo ambaye sasa amejifungua, alisema
shangazi yake ambaye hana msaidizi nyumbani kwake, alimpigia simu bibi
yake anayeishi naye, akimuomba yeye aende kumsaidia kufua nguo.
Alipokwenda, kwanza aliambiwa atoe mbolea katika zizi la ng’ombe lakini
akiwa huko, binamu yake, ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa, alimfuata
na kutaka kumbaka, kabla ya kufanikiwa kukimbia.
0 maoni:
Chapisha Maoni