Binti mwenye miaka 16
ametembea kwa miguu kilomita 100 kwa muda wa siku mbili kutoka Kijiji cha
Ighombwe hadi Singida mjini kuomba msaada baada ya mume aliyekuwa akiishi naye kumyanyasa
mara kwa mara
Binti
huyo kutoka wilaya ya Maswa, alifunga ndoa na Michael Luhende miezi tisa
iliyopita na kwamba mpaka hivi ana ujauzito wa miezi mitatu.
Binti
huyo aliyeozeshwa kwa mahari ya ng’ombe 16 na wazazi wake baada ya kufunga ndoa
alianza kuishi na mumewe huyo ambaye naye ni msukuma wa Kijiji cha Ighombwe, wilayani
Ikungi Mkoani Singida.
Amesema
ameamua kuchukua maamuzi ya kutoroka nyumbani baada ya kupigwa mara kwa mara na
mwenzake kutokana na sababu zizo za msingi
Wasamaria
waliomuokota akiwemo Bi Maria Daudi na Elizabethi Lazaro wamesema licha ya
msichana huyo kutokuwa na fedha za nauli wala chakula lakini hakuwa tayari
kurudi nyumbani kwake ili kuendelea kuishi na mumewe
Mratibu
wa Kituo cha Usaidizi wa kisheria cha SINGIDA PARALEGAL AID CENTRE,Bi Fatuma
Amiri amesema kuwa baada ya ofisi yake kupata taarifa za kufanyiwa ukatili
huo,wao walimfikisha Kituo kikuu cha Polisi mjini Singida kumtafutia msaada kwa kuwa binti
huyo hakuwa tayari kurudishwa kwa mumewe
Hata
hivyo Bi Fatuma amesema baada ya kumfikisha katika jeshi la polisi,jeshi hilo
kupitia kitengo cha usalama barabarani waliamua kumpatia kibali cha polisi ili
aweze kupata msaada wa usafiri wa kufika kwao Mkoani Shinyanga.
0 maoni:
Chapisha Maoni