Jumamosi, 16 Agosti 2014

      KOCHA mpya wa Simba,Patrick Phiri, ameshtuka kusikia kuwa Mbrazili Marcio Maximo aliyekuwa akiinoa Taifa Stars yupo Yanga kwa sasa na atalazimika kukumbana naye timu hizo zitakapokutana kwenye mashindano mbalimbali yatakayozikutanisha msimu ujao.
Phiri akizungumza na Mwanaspoti hotelini alipofikia jijini Dar es Salaam jana Alhamisi, alionekana kushtuka alipoulizwa juu ya Maximo na akasema: “Kwani bado yupo Tanzania? ni kocha wa Yanga kumbe?”
Aliongeza kuwa Maximo ni rafiki yake na wanaheshimiana sana, lakini kwa sasa Mbrazili hiyo hana jinsi itabidi aishuhudie timu yake ya Yanga ikimaliza nyuma ya Simba.
Wakati Phiri akiwa kocha wa Simba msimu wa 2009/10 timu hiyo ilipomaliza msimu bila kufungwa, Maximo alikuwa akiifundisha Taifa Stars hivyo walikuwa wakifanya kazi kwa karibu ili kuisaidia timu hiyo ya Taifa, lakini sasa mambo yamegeuka kwani makocha hao watakuwa wakifundisha timu mahasimu.
Yanga ni timu nzuri, inacheza mpira mzuri lakini itabidi wakubaliane na uhalisia kuwa Simba inarudi kwenye hadhi yake na Yanga italazimika kumaliza nyuma yetu, hiyo ndiyo njia pekee,” alisema Mzambia huyo.
Binafsi nadhani wafurahie sisi kuwa mbele yao kwa sababu wakizubaa wanaweza kuwa tena nyuma ya timu nyingine, mechi tutakayokutana itabidi nihakikishe nawafunga, hapo ndipo mashabiki wa Simba wanapasubiri.”
Kocha huyo ana heshima kubwa Msimbazi baada ya kuipatia ubingwa mara mbili na kuisaidia timu hiyo kumaliza msimu bila kufungwa ambapo baada ya kuondoka kwake klabu hiyo ilifanikiwa kufanya vizuri kwa msimu mmoja pekee kabla ya kuporomoka na kumaliza kwenye nafasi ya nne msimu uliopita.


Wapenzi wa Simba wanaweza wasimwelewe Phiri kwa hili kutokana na klabu ya Manchester United kumaliza katika nafasi ya saba msimu uliopita, lakini kocha huyo amesema anataka kuitengeneza klabu hiyo iwe kama Manchester United iliyochukua ubingwa mwaka juzi.
“Hapa ni kama mnanikumbusha Manchester United, ni timu yenye heshima, kikosi chake kimetengenezwa kwa muungano ambao unaisaidia timu kufanya vizuri kwa nyakati zote, hivyo ndivyo ninavyotaka Simba iwe,” alisema.
Kwa muunganiko huu, timu itaweza kufanya vizuri kila mechi, itaweza kutoka nyuma na kuongoza katika mechi, si rahisi kuona timu inapoteza mchezo wakati  imeunganishwa kuanzia nyuma hadi mbele, alisema Phiri.




BAADA ya kutua nchini, kocha wa Simba Patrick Phiri alishtuka kusikia Mbrazili Marcio Maximo yupo Yanga na sasa jamaa amemjibu Phiri akisema: “Ndio nipo Yanga nimejaa tele.” Akaendelea na mambo yake.
Maximo amesema ushindani mkubwa wa namba ulioko kwenye kikosi cha klabu hiyo umewafanya baadhi ya wachezaji wanaougua malaria kutaka kuendelea na mazoezi badala ya kupumzika.
Namfahamu kocha Phiri (Patrick), ni kocha mzuri, nilifurahi kufanya naye kazi kipindi nikiwa timu ya Taifa na yeye akiwa Simba, nina imani kuwa ujio wake utaongeza changamoto kwenye ligi na ubingwa utakuwa mgumu zaidi msimu ujao,” alisema Maximo
Akizungumzia wachezaji wake, Maximo alisema: “Ushindani wa namba kwenye kikosi changu umekuwa mkubwa, nafarijika kuona kila mchezaji anataka kucheza, hiyo inanipa imani kuwa nitakuwa na kikosi bora msimu ujao.”


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top