Jumanne, 19 Agosti 2014

         Mapigano kusitishwa kwa siku 1 zaidi


Isareli inataka kuzuia uingizwaji wa bidhaa za ujenzi ikihofia zitatumiwa dhidi yake.
Mpango wa kusitisha mapigano Gaza utaendelea kwa zaidi kwa saa ishirini na nne zijazo ilikupatia wajumbe wanaoendelea na mazungumzo muda zaidi wa kujaribu kutafuta suluhu la kudumu .
Kauli hiyo imeafikiwa na wapatanishi wa mazungumzo ya amani yanayoendelea huko Cairo.
Kwa mujibu wa taaraifa iliyotolewa na serikali ya Misri Jumatatu ''mazungumzo yaliendelezwa zaidi hadi jumanne ilikupatia pande zote muda zaidi wa mazungumzo''.
Viongozi wa Wapalestina walisema kuwa hakujakuwa na mapatano yeyote na kuwa walikuwa tayari kundelea na mapigano .
Kufikia sasa zaidi ya Wapalestina 2016 na Waisraeli 66 wameaga dunia tangu Israeli kuanza kuishambulia gaza Julai tarehe 8.

Wapalestina wanataka haki ya kuvua samaki baharini bila vikwazo vya Israeli
Kwenye taarifa iliyotolewa muda mchache kabla ya kukamilika kwa muda wa awali wa kusitisha mapigano usiku wa manane jumatatu,serikali ya Misri ilieleza kuwa pande zote mbili zilikubalian muda kuongezwa.
Kusitizwa kwa vita kulitekelezwa Jumatano.
Hapo awali waziri mkuu Benjamin Netanyahu alikuwa ameonya kuwa jeshi la Israeli lilikuwa tayari kulipiza kisasi mara tu hamas ingeanza kuishambulia Israili.
Mwakilishi wa Palestina Qais Abdul Karim alisema kuwa israeli ilikuwa inatafuta mbinu ya Hamas na maeneo mengine ya Gaza kupokonywa silaha bila ya kukubali matamanio ya hamas ya kutaka Israeli na Misri kuondoa vikwazo ilivyoiwekea Gaza.
Hamas wanataka vizuizi vya Israeli na Misri kuondolewa
Hamas inasema kuwa haitasalimisha silaha zake kwa Israeli ambayo inasisitiza kudhibiti biashara ya silaha Gaza.
Israeli inawasi wasi wa kuagizwa kwa vifaa vya ujenzi kuingia Gaza ikisema huenda Hamas wakatumia nafasi hii kujenga upya Handaki na njia za chini kwa chini.
Hata hivyo mjumbe wa katikati mashariki Robert Serry mnamo Jumatatu alisema kuwa umoja wa kitaifa ulikuwa tayari kusimamia ununuzi wa bidhaa za ujenzi Gaza kwa sababu nyumba nyingi makao ya familia nyingi zimeharibiwa katika operesheni iliyoendeshwa na Israeli.
Bwana Serry aliongeza kuwa Takribani nyumba 16,800 zimeharibiwa na wapelestina 100000 kuathirika na pia zaidi ya makazi 100 ya umoja wa kimataifa ya wahamiaji wapalestina kuharibiwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top