Ebola:IOC yazuia wachezaji wa Afrika
Wanariadha wanaotokea mataifa yaliyoathirika na homa ya Ebola
wamezuia kushiriki makala ya mwaka huu ya mashindano ya olimpiki ya vijana
yaliyoanza leo katika mji wa Nanjing Uchina.
Kamati andalizi ya mashindano hayo iliamua kuwatenga wanariadha watatu
kutoka Guinea na Nigeria kutoshiriki mashindano ya uogeleaji na yale yanayohusu
kugusana .Kamati ya olimpiliki duniani IOC ilisema kuwa ni vigumu kuenezwa kwa homa hiyo ya Ebola japo wanachukua tahadhari hiyo kwa maslahi ya washiriki wengine.
0 maoni:
Chapisha Maoni