Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uratibu wa Kanda wa
CHADEMA, Bw Benson Kigaila, amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi
wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo amesema zoezi la kuchukua na kurejesha fomu
kwa nafasi za kitaifa limeongezewa hadi Agosti 30 mwaka huu badala ya Agosti 25
iliyokuwa imetangazwa awali.
Amesema kuwa bado kuna chaguzi mbalimbali
zinafanyika ngazi za mikoa, hivyo sekretarieti ya chama hicho iliyokutana Dar
es Salaam juzi, iliamua kuongeza ili wagombea wengine watakaoshinda kwenye
ngazi za mikoa, wapate pia fursa ya kugombea nafasi mbalimbali za kitaifa.
0 maoni:
Chapisha Maoni