RONALDO AMGARAGAZA TENA MESSI, ABEBA TUZO YA MWANASOKA BORA ULAYA.
MRENO
Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya msimu wa
2013-2014 katika sherehe zilizofanyika jioni ya leo mjini Monaco,
Ufaransa.
Nyota
huyo wa Real Madrid amewapiku nyota wa Bayern Munich, kipa Mjerumani
Manuel Neuer na winga Mholanzi, Arjen Robben alioingia nao fainali.
Wakati
Neuer alishinda taji la Bundesliga na Kombe la Dunia msimu uliopita,
Robben alifunga mabao 22 kwa klabu na timu yake ya taifa msimu uliopita
na Ronaldo alifunga mabao 56 na kutoa pasi 15 za mabao Real Madrid na
Ureno. Mshindi wa mwaka jana, Mfaransa Franck Ribery hakuingia fainali.Ronaldo pia ni Mwanasoka Bora wa Dunia na ushindi huu ni pigo lingine kwa mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Argentina na Barcelona.
0 maoni:
Chapisha Maoni