BALOTELLI ATUA LIVERPOOL KUKAMILISHA USAJILI WAKE
MSHAMBULIAJI
Mario Balotelli alitarajiwa kuwasili England leo mchana kwa ajili ya
kufikia makubaliano ya kujiunga na Liverpool baada ya klabu hiyo
kufikia makubaliano na wawakilishi wake.
Mpachika
mabao huyo wa zamani wa Manchester City yuko karibu kusaini kikosi cha
Brendan Rodgers na amekwenda huko kukamilisha dili hilo mara moja.
Baada
ya kuwasili, Balotelli alitarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo katika
hospitali ya klabu hiyo, Spire Liverpool kabla ya kwenda kufanyiwa
vipimo zaidi vya afya katika viwanja vya Melwood vinavyotumika kwa
mazoezi na klabu hiyo.
Pamoja
na hayo, mshambuliaji huyo wa Italia hataweza kuichezea Liverpool dhidi
ya klabu yake ya zamani, Manchester City Jumatatu usiku, katokana na
muda wa usajili kwa leo kupita.
Anawasili: Mario Balotelli aliyepigwa picha hii mwaka jana, anatua Liverpool leo kukamilisha usajili wake
0 maoni:
Chapisha Maoni