MBEYA CITY FC UTANI MWIKO, MAANDALIZI YA MSIMU UJAO YAIVA
TAARIFA
zilizotufikia ni kwamba benchi la ufundi la Mbeya City fc
chini ya kocha mkuu, Juma Mwambusi akisaidiwa na Maka Mwalwisyi
linatarajia kufanya kikao mchana wa leo kwa lengo la kutathmini
walichovuna msimu huu.
Kocha
msaidizi wa Mbeya City, Maka Mwaliwisyi ameuambia mtandao huu kuwa
wamefurahishwa na mafanikio ya kushika nafasi ya tatu katika msimu wao
wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara, ingawa malengo yao ya kutwaa
ubingwa hayajatimia.
“Mchana wa leo sisi kama benchi la ufundi tunakutana ili kutathmini kile tulichokipata”.
“ Kulikuwepo na changamoto nyingi na tumemaliza nafasi ya tatu”.
“Tunakaa kwasababu tunatakiwa kuwasilisha ripoti mapema ili kuendelea na maandalizi ya timu”. Alisema Maka.
Kuhusu usajili, Maka alisema hawatahangaika na wachezaji wenye majina kwasababu falsafa yao inawabana.
“Wachezaji wetu wanatutosha. Tutapata wengine kwa njia ile ile tuliyotumia”.
“
Falsafa yetu inasema lazima tuwatoe wachezaji chini na kuwapandisha
juu. Tukisema tutamani basi tutapotea njia yeti tuliyoianzisha”
“Hawa
tulionao tutabaki nao ili tuone falsafa yetu itatufikisha wapi.
Hatusajili wachezaji wenye majina na ndivyo ilivyo kwa Mbeya City fc”.
Aliongeza Maka.
Mbeya City imekuwa timu bora msimu huu kwa kuleta changamoto kubwa kwa klabu za Simba, Yanga na Azam fc.
Katika msimu wake wa kwanza, wamewachomoa Simba katika nafasi tatu za juu.
Wamemaliza ligi katika nafasi ya tatu kwa pointi 49, huku nafasi ya nne ikiangukia mikononi mwa Simba kwa pointi 38.
Mwa jana, Yanga walitwaa ubingwa, Azam fc nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu, Kagera Sugar nafasi ya nne.
Lakini
mwaka huu Azam fc wametwaa ubingwa, nafasi ya pili Yanga, Mbeya City fc
ya tatu, Simba ya nne, na Kagera Sugar imeporomoka mpaka nafasi ya
tano.
Timu
nyingine zilizopanda na Mbeya City fc, kwa maana ya Ashanti United na
Rhino Rangers zimeshashuka daraja sambamba na JKT Oljoro.
Sasa nafasi zao zimechukuliwa na Stand United ya Shinyanga, Ndanda fc ya Mtwara na Polisi Morogoro ya Mkoani Morogoro.
0 maoni:
Chapisha Maoni