WANAMUZIKI MAARUFU BONGO WAZUNGUMZIA KIFO CHA MZEE NGURUMO..SOMA HAPA
Baadhi
ya Wasanii wa hapa nchini walizungumza na sammisago.com kwa njia ya
simu akiwa wakielezea juu ya kuguswa na msiba wa msanii nguli wa muziki
wa Dansi Marehemu Muhidin Gurumo aliyefariki jana tarehe 13 April
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Afande Sele:
“Ni
mamabo ya kumwachia Mungu na Mzee alishakuwa Mtu Mzima na alikuwa
anaumwa kwa muda mrefu, na hatuwezi kuongea kinafiki labda kama ni
mshtuko sana kama ilivyotokea kwa kina Kanumba, Albert ambao ni vijana
wadogo waliokufa bila kuugua yaani ghafla, Mzee Gurumo ni suala la
kumuachia Mungu ni kusema tunamshukuru Mungu kwa sababu yeye ndiyo
ametoa na yeye ndiyo ametwaa, na alishafanya kazi nyingi sana ambazo
zilimwekea heshima kubwa ndani na nje ya nchi, Kwa hiyo Mwenyezimungu
kampenda zaidi”

A.Y
Kwanza
hata mimi mwenyewe nilipata taarifa na msiba kuupokea kwa mshtuko na
kusema kweli ni mzee ambaye aliusukuma muziki tangu unavyoanza yaani,
enzi za kina Baraka Mwishehe, na walifuata kina Mzee Gurumo na vile
ambavyo mara ya mwisho nilimuona nilimchukulia kati ya wale watu ni
kwamba taswira halisi ya Muziki wa Tanzania na sauti yake naamini
itaishi miaka mingi sana na lamsingi ni kumwombea tu Mungu ampumzishe
mahala pema peponi na tuzidi kumwombea na kuenzi muziki wake pamoja na
familia yake na Band nzima ya Msondo”
Mwasiti:
“Kiukweli
mimi kama Mwanamuziki kama pia mwanamuziki Mchanga niseme hivyo,
Gurumo alikuwa Mwanamuziki Mkubwa sana, mimi niliweza kukutana naye kama
mara mbili hivi pale THT kwa hiyo nilipata nafasi hiyo kupitia pale ni
Mzee ambaye alikuwa anapenda watu na Mzee aliyekuwa anapenda Muziki wetu
wa Bongo Fleva, pia ni Mzee ambaye ukikaa naye anakuambia muwekeze
katika muziki kwa sababu aliona muziki wao na muziki wetu kuna tofauti
kidogo sasa hivi wanapata pesa ya maana, pia nilikuwa nasikiliza nyimbo
zake kwa muda mrefu sana tofauti na tunazozifanya sasa hivi kwa jinsi
zilivyokuwa zinatufundisha. Kiukweli tumepoteza Hadhina kubwa sana
katika muziki na inabidi tuende kwenye msiba tukawafariji familia ya
marehemu”
Kala Pina:
“Kwa
sisi ambao tupo kwenye tasnia nzima ya muziki ni pigo kubwa kwetu
kutokana na Mzee wetu Gurumo ni moja kati ya wanamuziki wakongwe ambao
wamefanya sanaa kwa miaka mingi na nyimbo zenye ujumbe wakuelimisha,
kiukweli ameacha pengo ambalo sidhani kama kuna kitu atakayeweza kuja
kuliziba katika tasnia nzima ya muziki, na ameweza kuweka histori kubwa
sana ya kudumu kwa muda mrefu kwenye muziki, mimi naamini tupo kwenye
msiba wasanii wote Tanzania nzima na tunaomboleza na tutakuwa wote
pamoja kuhakikisha tunamzika Mzee wetu”
Msiba
wa Marehemu Muhidin Gurumo upo numbani kwake maeneo ya Tabata Makubuli
na mazishi hapo kesho taraehe 15 April katika makaburi ya Masaki huko
Kisarawe Mkoa wa Pwani. Mungu ailaze roho ya Marehemu pema peponi Amen
BANDOLA.BLOGSPOT.COM
0 maoni:
Chapisha Maoni