Ni shabiki mkubwa wa Yanga ambae alipata zaidi ya shilingi milioni 4
kwenye miezi miwili ya kwanza baada tu ya kuonekana kwenye TV akilia kwa
uchungu kisa Yanga imefungwa tano, zikiwa ni pesa kutoka kwa watu mbalimbali
ambao walimuonea huruma na wengine kujisikia tu kumpoozesha.
Ni muda umepita toka hiyo mechi ambapo leo tena Yanga na Simba kwenye uwanja
wa taifa zinakutana ambapo Steven alipita mbele ya Camera ya millardayo.com na
kuzungumza machache kuhusu hii mechi ya leo.
‘game ya leo ni nzuri japo maandalizi tumeshaanza muda mwingi sana
tumejiandaa vizuri kwa hiyo tunategemea na sisi kupata ushindi sana,
hatutegemei kama tutaipoteza hii game’ – Steven
Leo mkifungwa utalia tena? ‘leo
nikifungwa ndio nitazimia moja kwa moja na kuna uwezekano nikaihama hata club
kwa sababu imani yangu iko hapa tayari kwamba tutashinda ila tukifungwa tena
nitaachia ngazi kistaarabu, nitamuandikia barua Muheshimiwa Manji manake yeye
ndio alinipa cheti cha heshima cha uwanachama wa Yanga, kuhusu club gani
nitahamia hiyo ni siri yangu’ -Steven
‘Yanga sasa hivi tuko kiprofeshino kama Barcelona sasa hivi au Real
Madrid, Simba tutaiona manake imesajili sana mwaka huu kama kina Tambwe…. kwa
hiyo tunategemea maushindi zaidi utakuepo, tena ushindi wa mawili kwa moja au
moja bila… si hatuhitaji magoli matano, tunahitaji pointi tatu tu’ – Steven
Jumapili, 20 Oktoba 2013
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni