Ufoo Saro: “Nyumbani kwetu, pale Kibamba si mbali
sana na barabarani, wakati nikikaribia kufika barabarani wakati huo nikitokwa
na damu nyingi huku nikihisi tumbo langu limejaa sana nilikutana na dada mmoja
ambaye nilimuomba khanga ili nijifunge kuzuia damu zisitoke kwa wingi”.
Anasema dada yule alimpa khanga akajifunga na
aliposogea barabarani alikutana na gari lililokuwa likiendeshwa na mwanamke
mmoja.
“Nilipoona kuna gari linapita nikainuka kuomba msaada.
Liliposimama nilimuona mwanamke akiendesha nikamweleza kwamba nilikuwa
nimepigwa risasi na nilikuwa nikiomba msaada wake anikimbize hadi katika
hospitali ya Tumbi na kwamba akifika pale tu aniache mlangoni..
Liliposimama nilimuona mwanamke akiendesha
nikamweleza kwamba nilikuwa nimepigwa risasi na nilikuwa nikiomba msaada wake
anikimbize hadi katika hospitali ya Tumbi na kwamba akifika pale tu aniache
mlangoni.
“Si rahisi kuamini, yule mama alikataa kunisaidia
akisema alikuwa akiwahi sehemu kumchukua mzazi. Sina la kusema niliamua
kumsamehe tu yule mama ingawa niliumia sana,
0 maoni:
Chapisha Maoni