Yanga
Kampuni yazua mtafaruku Jangwani
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, alisema jana
Jumatano kuwa wanachama hao watatoa maoni kama wanataka Yanga iwe kampuni au
iendelee na mfumo wa sasa wa wanachama.
“Wanachama wa Yanga wanatakiwa kutoa maoni yao kwa kupiga
kura za ndio au hapana kwenye sanduku la maoni ambalo litakuwa hapa klabuni,”
alisema Mwalusako ambaye Mwanaspoti linajua Mkenya, Patrick Naggi atapewa
nafasi yake.
Alisema utaratibu huo utafikia tamati Novemba 10 na kwamba
mwanachama atalazimika kupiga kura kwa kadi yake ambayo ameilipia, kwani
itamthibitisha kuwa ni mwanachama hai na atatakiwa kupiga kura mara moja.
Hata hivyo, wakati Yanga wameanzisha utaratibu huo, Yanga ni
klabu pekee, ambayo imeshasajiliwa na Msajili wa Makampuni tangu Juni 28, 2000.
Kampuni hiyo ilisajiliwa na kupewa namba 39551 chini ya Francis Kifukwe na
ilifikia hatua ya kuuza hisa zake.
Malinzi alishangaa kusikia mchakato huo umetangazwa na
kusema: “Yanga siku nyingi sana ilishakuwa Kampuni na tulifikia hatua ya kuuza
hisa zake, kilichopo sasa viongozi waliopo wanatakiwa kuendeleza pale
tulipoishia kama kweli wana nia ya kuendesha kklabu hiyo kisasa kwa mtindo wa
kampuni.”
Malinzi alisema yeye ni mmoja wa wana hisa kwenye kampuni
hiyo ya Yanga, wengine ni Francis Kifukwe, Ibrahim Didi, Abbas Tarimba na David
Lwimbo.
Kuelekea mchakato huo kulizuka mgogoro mkubwa na kuigawa
Yanga vipande vitatu; Yanga Kampuni iliyokuwa chini ya Kifukwe, Yanga Asili
chini ya Yusuph Mzimba na Yanga Academia iliyokuwa chini ya Costantine Merinyo
‘Kibo’.
0 maoni:
Chapisha Maoni