Aliyefungiwa miaka 20 aivimbia TFF
RICHARD Rukambura anatembea na rufaa yake mkononi na ndani
ya siku mbili atatinga Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga adhabu ya kufungiwa
kujihusisha na soka kwa miaka 20.
Rukambura amefungiwa kwa muda huo na Kamati ya Maadili ya
Rufaa baada ya kupeleka masuala ya soka katika mahakama za kawaida kinyume na
Ibara ya 75 ya Katiba ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kifungu cha 73
(3) (b) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013. Adhabu yake itamalizika
Oktoba 15, 2033.
Rukambura amekumbwa na adhabu hiyo baada ya kufungua kesi
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuenguliwa kwenye uchaguzi wa awali wa
shirikisho hilo uliokuwa ufanyike Februari 23 mwaka huu.
Hata hivyo, uchaguzi huo ulifutiliwa mbali na shirikisho la
kimataifa la mchezo huo, Fifa, baada ya
baadhi ya wagombea kuenguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho na kupeleka
malalamiko yao huko. Fifa iliingilia kati na kufuta mchakato mzima wa uchaguzi
na kuagiza mchakato uanze upya na
Lakini jana Jumatano Rukambura alisema: “Sitakubali kukatwa,
kama ‘mbwai na iwe mbwai’ nitahakikisha nakata rufaa mahakamani ndani ya siku
mbili hizi, kwa vile ndicho wanachokitaka TFF ili waendelee kubaki madarakani.
“Nimesema sikubali, kamati ya maadili ambayo ilinisafisha
ina majaji na mawakili, hiyo kanuni ya kunifungia sikubaliani nayo,
nitahakikisha haki yangu naipata mahakamani.
“Katiba ya TFF imesajiliwa na msajili wa vyama vya michezo
kwa sheria ya nchi iliyotungwa na Bunge na si kanuni za Fifa, wanapaswa
kuheshimu vyombo vya mahakama, mimi nitakwenda mahakamani liwalo na liwe.”

0 maoni:
Chapisha Maoni